Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Seleman Jafo ameziagiza Halmshauri zote
hapa nchini kupanda miti isiyopungua Milioni moja na laki tano kila mwaka
kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo husababisha madhara makubwa ikiwemo
uharibifu wa Mazingira
Waziri Jafo ametoa maagizo
hayo leo jijini Dodoma wakati zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Medeli
lilipo jijini hapa, amesema hivi sasa hali ya hewa imebadilika katika maeneo
mbalimbali kutokana na uharibifu wa mazingira huku maeneo mengine yakiwa ni
makame.
‘’upandaji huu wa miti
unatusaidia sana kuhakikisha tunarekebisha mabadiliko ya tabia ya nchi’’amesema
Jafo
Aidha, Waziri Jafo amesema
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wameanzisha kampeni kabambe
ya Usafi wa Mazingira na Utunzaji wa Mazingira kukabiliana na mabadiliko hayo.
"kampeni hii ili
itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Philip Mpango
tarehe 5 ya mwezi wa 6 na tunataka Tanzania iwe nchi ya mfano Duniani kokote
mtu akitoka anakuwa anatamani kuja hapa kutokana na Mazingira yaliyopo’’
amesema Jafo
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema kwenye ajenda kama Mkoa ni kuhakikisha kuwa Mazingira yanakuwa ya kijani.
"Kama viongozi wa Mkoa tutatekeleza maelekezo
yatakayotolewa na Ofisi ya makamu wa Rais
Muungano na Mazingira na tuko tayari kwa
jambo hili ambalo limeanzishwa na litatekelezeka’’ amesisitiza Mtaka
Kamishna Mhifadhi Misitu
Profesa Dos Santos Silayo ameahidi kushirikiana kwa kuifanikisha kampeni hiyo
kwa uadilifu mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kampeni hiyo.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Dodoma Antony Peter Mavunde amesema kutokana na hali ya hewa ya Dodoma
inahitaji muamko mkubwa wa upandaji miti huku akiahidi kuwa kampeni hiyo inafanikiwa
kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Hatahivyo, kampeni hiyo
ambayo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataizindua June 5
kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani, Waziri jafo aliteua Wajumbe 14
washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye lengo la
kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi shindani Duniani katika utunzaji wa
Mazingira.
CHANZO; DODOMA NEWS
0 comments:
Post a Comment