METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 1, 2021

RAIS SAMIA :TUTAONGEZA MISHAHARA MWAKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wafanyakazi mbalimbali katika Kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi Kitaifa ambazo zimefanyika Jijini Mwanza leo tarehe 01 Mei, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,ameahidi kuwa mwakani siku kama ya leo atapandisha mishahara kwa watumishi .

Rais ametoa kauli hiyo Leo Mei Mosi wakati akihutubia wafanyakazi katika Ameyasema  maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa yaliyofanyika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

“Ndugu zangu mimi ni mama, mama ni mlezi,Dai hili ni la msingi na la kweli. Mishahara haijaongezwa muda mrefu. Kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona uwezo wetu kiuchumi umepungua, imekuwa vigumu kwangu kuongeza mishahara lakini tutaboresha maslahi ya wafanyakazi”, amesema Rais Samia.

“Mishahara haijaongezwa kwa muda mrefu, Mimi binafsi natamani kuongeza mishahara mwaka huu ila kwasababu mbalimbali nimeshindwa, uchumi wa Tanzania umeshuka kutoka 6.9% hadi 4.7% kwasababu ya Corona, nawaahidi mwakani siku kama ya leo nitapandisha mishahara”, amesema Rais Samia.

Hata hivyo Rais Samia amesema  kuwa jumla ya wafanyakazi zaidi ya 85,000 elfu hadi 91,000  watapanda vyeo mwaka ujao na  kuajiri watumishi  40,000 katika Idara ya Elimu na Afya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com