Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akifanya tathmini ya hali ya lishe ( uwiano wa urefu na uzito) wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa.Kulia ni Mtaalam wa Chakula na Lishe toka Shirika la Sema Singida Tito Mkemwa( aliyeshika kitabu).
Mkuu wa
Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akisaini kitabu wakati
alipotembelea banda la mradi wa Kudhibiti Sumu Kuvu kwenye nafaka (TANIPAC)
kwenye maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.Kushoto ni Mohamed Chikawe
mwakilishi wa Mratibu toka Wizara ya Kilimo.
Na Revocatus Kassimba, Wizara ya Kilimo-Singida
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi leo Ijumaa tarehe 11 Octoba,2019ametembelea mabanda ya
maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa katika uwanja wa
Bombardier,Manispaa ya Singida.
Amesema uwepo wa maadhimisho haya ni fursa kwa wananchi wote kutambua umuhimu
wa lishe bora kwa afya .
Amebainisha kuwa elimu juu ya uandaaji chakula tangu kikiwa shambani,baada ya
mavuno,wakati wa kukiandaa nyumbani na wakati wa kupika inatakiwa ili mwananchi
ale mlo kamili na bora.
Mhe.Dkt.Nchimbi amewasihi wataalam wa lishe nchini kutoa elimu sahihi kwa
wananchi kuelewa makundi muhimu ya
chakula kinachopaswa kutumiwa na binadamu.
"Uwepo wa maadhimisho haya ya kitaifa Singida usaidie jamii kutambua
umuhimu wa lishe bora kwa ustawi wa afya za watu ili washiriki kikamilifu
katika ujenzi wa taifa"Mhe. Nchimbi
Aidha,amewasihi Mkuu huyo wa mkoa amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi
kupata elimu juu ya lishe bora na teknolojia rahisi ya kuongeza thamani ya
mazao ya chakula.
Uzinduzi
rasmi wa maadhimisho hayo utafanyika Jumapili ijayo na yatahitimishwa tarehe 16
mwezi huu.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni " Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio
na Njaa".
0 comments:
Post a Comment