METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, May 23, 2021

MBUNGE WA JIMBO LA NACHINGWEA AKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA MILLION 22


Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile amekabidhi mifuko ya saruji 1,800 Mei 22 /2021 ikiwa ni Moja ya  ahadi yake katika sekta ya  ELIMU  aliyoitoa wakati akiomba ridhaa katika uchaguzi Mkuu 2020.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika kata 16  kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule za sekondari ndani ya kata hizo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Amandus Chinguile alisema 'yeye kama Mbunge anao wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kuwaboreshea miundombinu.

Alisema kuwa ataendelea kuziangazia shule zenye changamoto na kuziwekea mazingira rafiki ya kujifunzia.

Vifaa hivyo vinatarajia kutumika kakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa  22 katika Shule za Sekondari zilizopo Jimboni humo.

"Ni wajibu wetu sisi kama viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja   kuinua Elimu katika wilaya yetu kwa kuhakikisha tunaiboresha Miundombinu ya shule"Alisema Chinguile. 

Aliongeza kuwa, hii awamu ya kwanza  ameziangazia kata 16 katika sekta ya Elimu,akini ataendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika kata nyingine.

'Ili Jimbo  liendelee kupiga hatua kimaendeleo nitaendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi  kwa kuimarisha miradi ya Maendeleo katika sekta ya Maji,Afya ikiwemo kuisimamia Serikali katika sekta ya Kulimo ili pembejeo za Kilimo ziweze kuwafikia kwa wakati na zipatikane kwa bei nafuu.

Akiiangazia sekta ya Elimu alisema,bado hitaji ni kubwa hivyo ni jukumu la kila mdau kuendelea kuchangia ili changamoto zinazoikabili sekta hiyo ziweze kumalizika na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki ili kuongeza ufahuru.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com