Na Anitha Jonas – COSOTA,Dar es Salaam
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imefanya operesheni katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa kazi za Filamu na Muziki na ambapo kukamata zaidi ya mashine 50 zenye uwezo wa kudurufu takribani nakala 10,000 kwa nusu saa.
Operesheni hiyo ya uharamia wa kazi za Muziki na Filamu imefanyika Mei 18, 2021 Kariakoo, Jijini Dar es Salaam ambapo takribani watuhumiwa kumi na moja wanafanya shughuli za uazalishaji wa kazi haramu za filamu na Muziki walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
“Kifungu cha 42 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kamakilivyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 3 ya mwaka 2019 kinasema ukikamatwa kwa kosa la uvunjifu wa Hakimiliki faini yake ni isiyopungua milioni ishirini au Kifungo cha Miezi sita na kisichozidi Miaka Mitatu au vyote kwa pamoja”alisema Bw.Mwambinga.
Pamoja hayo Mwanasheria huyo alitoa onyo kali kwa wazalishaji wote na wasambazaji wa kazi za Muziki na Filamu ambao wanaburn CD za Muziki na Filamu, wanaoweka Muziki kwenye flash kwa kusema kuwa hilo ni kosa, na alisisitiza kuwa COSOTA imedhamiria tutahakikisha tunathibiti hilo na kwa yoyote atakayekamatwa na kazi hizo zisizo na mikataba au makubaliano na wamiliki atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Halikadhalika Bw.Mwambinga alifafanua kuhusu udurufu wa Filamu za nje bila kufuata utaratibu kuwa ni kosa na aliwasihi wazalishaji hao kuachakudanganyana, kwa kusema udurufu au uzalishaji wa kazi za nje bila kibali cha mmiliki unaruhusiwa,hivyo alisisitiza katika uuzalisha au udurufu wa kazi yoyote iwe Muziki au Filamu ya ndani au ya nje ya nchi ni lazima kuhakikisha kuwa unamakubaliano au mikataba na mmiliki wa kazi hiyo kinyume na hapo huo ni uharamia na uvunjifu wa Sheria ya Hakimiliki.
0 comments:
Post a Comment