METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 3, 2021

BASHUNGWA Amuwakilisha Rais Samia Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari




Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini inayofanyika leo  Mei 2021 Jijini Arusha.


Katika Maadhimisho hayo Mhe.Bashungwa ameeleza kuwa ni muhimu kwa Vyombo vya Habari kuwa na Mpango wa Maendeleo utakaowezesha vyombo hivyo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.


"Serikali inahimiza wadau wote wa Habari,Kuhakikisha wanaweka utaratibu unaowezesha kufanya ufuatiliaji na uwajibikaji katika kutekeleza Sera,na Sheria za nchi.Miongozo hiyo itazingatia kuwepo kwa mazingira na hali bora ya kazi, ulinzi na usalama wa waandishi, kujua kufanya kazi za uandishi pamoja na uelewa wa matumizi ya kijiditali" amesisitiza Mhe.Bashungwa.


Aidha  Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Viongozi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari pale inapohitajika kwa manufaa ya Umma na Maslahi ya Taifa letu kwa ujumla.

MWISHO.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com