“Nimefurahi sana kutembelewa na wasanii wetu Bungeni. Yale tuliyozungumza pamoja msiwe na shaka yatafanyiwa kazi. Mhe Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anawapenda wasanii wetu na ana imani kubwa na uwezo wenu wa kuitangaza vyema nchi”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema hayo katika ukurasa wake wa Twitte na kuongeza kuwa
“Nawaomba wasanii wote nchini tujenge tabia ya kujiheshimu na kuheshimiana. Mawili hayo yakifanyika tunakuwa na tasnia ya sanaa inayoheshimika machoni mwa watanzania na duniani. Natoa wito kwa wasanii wote kote nchini kuzingatia hili”
0 comments:
Post a Comment