Na Happy Severine, Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka ameshtukia mchezo mchafu wenye viashiria vya rushwa kwenye mradi wa JENGA UWEZO PROJECT
unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa,
vinavyofanywa na wataalamu wa shirika hilo kwa kushirikiana na watumishi wa
serikali.
Mtaka alishtukia mchezo huo baada ya kubaini
kuwepo kwa baadhi ya vipengele vya utekelezaji katika andiko la mradi, kutofanyika kama inavyotakiwa na badala yake
vimerukwa na kutekelezwa vipengele vya mbele, wakati fedha zake zipo.
Mkuu huyo aliyabaini hayo jana wakati wa kufungua kikao cha mradi huo unaogharimu kiasi
cha shilingi Milioni 595,738,099.12
kilichowahusisha kikihusisha
Wakurugenzi watendaji,Maafisa Utumishi ,Waganga wakuu wa Halmashauri za wilaya
zilizopo mkoani hapa,na kuonekana kushangazwa na kitendo cha AMREF kutofuata mtiririko wa
andiko la shughuli za mradi kama ilivyo pangwa na kuridhiwa na mfadhili ambao
ni Irish Aid,Rialtas ,Heireann ya serikali ya Ireland.
Aidha Mkuu huyo ameonya na kusema kuwa tabia
hiyo ni sawa na usanii kwa jamii ambao
unafanywa na baadhi ya watumishi wa serikali licha ya mkoa huo kuwa kuwa mpya kamwe wasije kufanya kuwa ni kichaka cha wizi wa fedha za wafadhili hali
inayoipaka doa serikali ya awamu ya tano
machoni mwa wafadhili.
Sambamba na hilo Mtaka amemkataa msimamizi wa mradi kutoka wizara ya
afya aliyeteulia na katibu mkuu wa wizara ya Afya kwa kile alichoeleza kushindwa kazi huku
akimuagiza mganga mkuu wa mkoa Mageda Kihulya kuandika bara mara moja na kuipeleka wizarani ya
kubadilishiwa msimamizi huyo.
Hata hivyo Kauli hiyo ilisababisha Dk, Ama Kasangala toka Wizara ya afya aliyepewa mamlaka ya kusimamia mradi huo kuangua kilio mbele ya wajumbe katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Sunga mjini Bariadi, huku Mkuu wa Mkoa akisema fedha hizo zinataka kuliwa na watumishi hao kinyume na utaratibu .
“inasikitisha sana na haiingii akilini kuona mkataba unaendeshwa ndivyo sivyo…na kwamba yeye kama msimamizi mkuu wa shughuli zote za maendeleo mkoani humo hawezi kuona fedha za wafadhili zikichezewa ovyo kupitia mkoa kwake… Alisema
Alisema kuwa tangu Desemba 2016 hadi Juni 2017 utekelezaji wa mradi huo katika mkoa mzima umekuwa na kazi kubwa ya kufanya mikutano mafunzo na semina ambazo alidai ni za ubabaishaji tu badala kutekeleza andiko hilo ambalo limelenga kutoa msaada juu ya afya ya jamii kupitia sera na Wizara kuridhia utekelezaji wa mradi huo katika huo ulioanzishwa mwaka 2012.
“Ninashangaa katika ratiba yenu kuna kukutana na wenyeviti na watendaji wa vijiji na kata zaidi ya 500 na madiwani mkoa wa Simiyu ambao ndiyo walengwa na ndio wenye watu lakini hapa kuna wawakilishi wa DEDs,DMOs, DHRs huu ni ubabaishaji tu mnakaa huko Dar es salaam mnapanga wapi mkapige fedha mnaona ni hapa Simiyu hilo halikubaliki”
Akitoa mfano halisi alisema kuwa hivi karibuni katika ziara ya Rais John Magufuli iligundulika kuwepo kwa mchezo mchafu wa kutaka kuhujumu mabilioni ya fedha za ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Simiyu ambapo Rais alistukia kiasi kilichoombwa kujenga hospitali ya Rufaa ya mkoa kwa gharama zaidi ya shilingi bilioni 46 badala bilioni 10 hivyo wapiga dili mkoani simiyu wajiandae kuondoka maana hata weza kuwavumilia.
Hata hivyo Mkuu huyo alisema kuwa ili mradi huo uweze kutekelezwa ni sharti ufuate na kuzingatia andiko la Mradi huo na kuitaka Amref kuanza utekelezaji wake na kukamilisha kama ulivyo kusudiwa ikiwahusisha walengwa wote kama andiko lenu lilivyo.
0 comments:
Post a Comment