Kutokana
na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua
kwa Rais Dk. John Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, awe
amepata nakala ya barua hiyo.
Agizo
hilo alilitoa jana baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Wilaya
ya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri
Mkuu alirejea Babati akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za
kitaifa.
“Nilikuja
kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki
huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa
mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya
kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi
inatoka Tanzania.
“Ni
kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya
Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa
nini Tanzania haionekani? kwani malighafi iko Kenya? haiwezekani, ni
lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye
anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya
hivyo?,” alihoji.
Akiwa
ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea
ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali
ya Kenya na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda
cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200
Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu
+254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.
Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.
Alisema
atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
kwenda kiwandani hapo na wanasheria wake pamoja na wataalamu kutoka Tume
ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waangalie hatua gani zinapaswa
kuchukuliwa.
“Kwa
staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia
upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa
imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” alisema
“Tukiruhusu
hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani
kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza
nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?,”
alisema na kuhoji
Akitoa
maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Tosky Hans
alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na
makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na
kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.
0 comments:
Post a Comment