Serikali imesema haitokubali waandishi wa habari nchini kunyanyawaswa kwa namna yoyote ile.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 16 Machi 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg GERSON MSIGWA mbele ya waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt Hassan Abass ikiwa ni mwanzo rasmi wa majukumu yake mapya.
Pia, Msigwa ametoa angalizo kwa waandishi wa habari kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayoongoza tasnia ili kuepuka sintofahamu inayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Pamoja na kuwataka waandishi wa habari nchini kutotumika kuibomoa nchi yao pia ametoa mwito kuhakikisha wanakuwa vinara wa kuijenga Tanzania.
Kwa upande wake aliyekuwa msemaji mkuu wa Serikali Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abass amewashukuru waandishi wa habari, Wadau na Watanzania wote kwa ujumla kuunga mkono juhudi za serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment