METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 10, 2020

KAMPENI ZA CCM VWAWA ZANOGA, NYOMI LA WANANCHI KAMA LOTE, HASUNGA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KAZI ITAENDELEA

Mgombea ubunge Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Japhet Hasunga akisoma ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2020 wakati wa ufunguzi wa kampeni mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020.

Sehemu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Jimbo la Vwawa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kampeni mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020. 

Mgombea ubunge Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Japhet Hasunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020.

Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Dkt. Edmund Ndolwa akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Japhet Hasunga wakati wa ufunguzi wa kampeni mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020.

Mgombea ubunge Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Japhet Hasunga pamoja na mgombea ubunge kupitia Viti maalumu Mkoa Songwe Juliana Shonza wakifurahia ngoma ya asili mara baada ya ufunguzi wa kampeni mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020.

Mgombea ubunge kupitia Viti maalumu Mkoa Songwe Juliana Shonza akiwananga wapinzani wakati wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori Tarehe 9 Septemba 2020.

Na Mwandishi Wetu, Songwe

Mgombea ubunge Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Japhet Hasunga amezindua rasmi kampeni na kueleza vipaumbele vyake ambavyo atavitekeleza iwapo atachaguliwa kuwa mbunge ambavyo ni pamoja na kuimarisha sekta ya Elimu, miundombinu, Afya na Elimu ya juu kadhalika ufundi stadi.

Uzinduzi huo ulifanyika Tarehe 9 Septemba 2020 mjini Vwawa katika viwanja vya stendi ya malori, ambapo Hasunga alisema iwapo akichaguliwa atahakikisha shule za kidato cha tano zinaongezeka kutoka 1 ya sasa na kukamilisha shule tatu zilizojengwa mwaka huu huku akiahidi kuisimamia serikali na kujenga nyingine moja ili ziwe shule tano ifikapo mwaka ujao wa 2021.

Amesema kuwa endapo wananchi wataendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kitaisimamia serikali kuendelea kuongeza zaidi shule za msingi na sekondari ili kuwaokoa watoto wanaohitimu kidato cha nne ambao wanakosa nafasi ya kuendelea na masomo kutokana uhaba wa shule za kidato cha tano.

Alisema ili kuufanya mji wa Vwawa kuwa wa kibiashara iwapo akichaguliwa atahakikisha anapambana kushawishi kuanzishwa kwa chuo kikuu walau kimoja na chuo cha ufundi VETA ambavyo vitaongeza idadi ya watu na kufanya biashara kuchangamka kwenye mji wa Vwawa.

Katika sekta ya Afya, Hasunga alisema atahakikisha vituo vya Afya zaidi vinajengwa kutoka vituo vya afya vitatu vya sasa ili viongezeke pia vipate madaktari na waganga huku akisisitiza kuwa atahakikisha madaktari bingwa wa kutosha wanapatikana katika hospitali ya rufaa ya Mkoa.

Mgombea huyo wa ubunge akizungumzia miundombinu ya barabara katika mji wa Vwawa alisema Mbozi ni moja ya wilaya ambayo IPO kwenye mpango wa uboreshaji wa miji (Strategic Cities) ambapo barabara nyingi za mitaa zitajengwa kwa kiwango cha Lami, ikiwemo ujenzi wa stendi kuu ya kisasa ya mabasi na soko la kimataifa katika eneo la Mbimba lilotolewa na Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Kuhusu Kilimo Hasunga alisema wataendelea kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati na bei nafuu na kuachilia soko huria kwa kutopanga bei za mazao na bila kufunga mipaka.

Kwa upande wake mgombea ubunge kupitia Viti maalumu Mkoa Songwe Juliana Shonza alisema ilani ya CCM inajieleza vizuri hivyo haihitaji kutumia nguvu kuisemea bali chama hicho kinatarajia ushindi mkubwa na kuwataka wananchi wa Vwawa kutofanya mzaha kwani sumu haionjwi kwa kuilamba.

Katika uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Dkt. Edmund Ndolwa ambaye aliwataka watanzania kuipigia kura CCM kwani ndicho chama chenye Sera yenye maslahi mapana ya umma na si vinginevyo.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com