METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 22, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan aongoza viongozi mbalimbali wa Ndani na Nje ya Nchi kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa na Viongozi wa  Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali Duniani kwenye Mazishi ya Kitaifa ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma leo March 22,2021.

 

Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kwa ajili ya shughuli ya kuagwa Kitaifa leo tarehe 22 Machi 2021. 

Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wakiwasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma 

Makamanda wa JWTZ wakipiga Saluti mara baada ya kuweka Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika chumba maalumu kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na viongozi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma 

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Felix Tshisekedi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma 

Rais wa Zambia Edgar Lungu akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma   

Mama Janeth Magufuli Mjane wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli akilia kwa uchungu wakati akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la mme wake katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com