METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 8, 2021

MAMA SALMA KIKWETE APEWA UGENI WA HESHIMA SIKU YA WANAWAKE MANISPAA YA LINDI




Katika kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mama Salma Kikwete amepewa heshima ya kuwa Mgeni wa Heshima kwenye hafla hiyo kwa kutambua mchango wake kwenye masuala mbalimbali ya Wanawake. Mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Rehema Madenge


Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mama Salma Kikwete amezungumza na Wanawake waliojitokeza kwenye sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambapo kwa ngazi ya Manispaa ya Lindi yamefanyika katika viwanja vya Mpira wa Kikapu (Bwalo la Polisi), amewataka Wanawake kushiriki kikamilifu katika kumtetea mtoto na kamwe wasikubali watoto wao kukatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com