METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, March 16, 2021

COSOTA na BASATA zaagizwa kukamilisha Mfumo wa uuzaji kazi za Sanaa Mtandaoni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akitoa maelekezo kwa COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao kufuatia ukuaji wa teknolojia na uwanda mpana wa masoko katika mfumo wa mtandao au  programu za  simu ’Apps’  leo Machi 15,2021 Jijini Dar es Salaam katika kikao wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilicholenga  kutatua changamoto zinazowakabili.

Afisa Mtendaji  Mkuu  wa Taasisi ya Hakimiliki  na Hakishiriki Tanzania Doreen Sinare akiwasisitiza  wanachama wa Tingatinga Arts kusajili kazi zao badala ya kusubiri mpaka wanapopata changamoto ndiyo wanakumbuka kujisajili, katika kikao na wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji  kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam leo Machi 15,2021  kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw.Andrian Nyangamale akitoa ombi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa kwa niaba ya Wasanii wa Sanaa ya Ufundi kuwa wanaomba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  anapokuwa akitoa zawadi ya Sanaa hizo kwa wageni  kutaja jina la Mchoraji au Mchongaji wa kazi hiyo kwa lengo la kusaidia kumtangazia biashara , leo  Machi 15,2021 Jijini Dar es Salaam katika kikao na wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilicholenga  kutatua changamoto zinazowakabili. 

Katibu wa Tingatinga Arts Tanzania Bw. … akiwasilisha akimwomba Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa kumsaidia kutatua changamoto ya mgogoro wa mipaka ya Kiwanja cha  Ofisi yao  Oysterbay leo  Machi 15,2021 jijini Dar es Salaam katika kikao wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kwa kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili. 

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (aliyeketi wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa Sanaa ya uchoraji na uchongaji mara baada ya kikao  na wadau hao kilichofanyika leo Jijijini Dar es Salaam kilicholenga kujadili changamoto zinazowakabili, aliyeketi ni watatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare.

Na Richard Mwamakafu – WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza COSOTA na BASATA kuandaa mfumo utakaosadia wasanii kuuza kazi zao mtandaoni.

Mhe.Bashungwa ameyasema hayo Machi 15, 2021 alipokutana na  Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) na Uchoraji (Tingatinga) ili kujua na kujadili Changamoto zinazowakabili ambapo ameahidi kuzifanyia kazi.

“Inabidi kushirikiana na vyama hivi ili kutengeneza platform ya mitandaoni ili kuuza bidhaa lakini nakulinda kazi za wasanii hawa, tuliahidi kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuanzisha mfuko wa sanaa na kwa habari iliyo njema kwa maelekezo ya Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli mfuko huu umeuwishwa sasa tunaanza kuutengea fedha kwa Mwaka huu wa Fedha 2021/2022 ambayo Bunge litakaa kwaajili yakuijadili hiyo bajeti lakini matarajio yetu kuanzia mwezi Julai angalau huu Mfuko uanze kuwa na Fedha kwaajili yakutoa mkopo kwa Wasanii wetu” alisema Mhe.Bashungwa.

Mheshimiwa Bashungwa aliwahakikishia wasanii hao kuwa serikali iko nao bega kwa bega katika kuisimamia sekta hiyo ya sanaa na kuahidi kuwa  serikali ipo tayari kusikiliza na kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA)

Bibi.Doreen Sinare alieleza kuwa taasisi hiyo imetengeneza Kanuni mpya ambazo zitawasaidia

Wachoraji na Wachongaji kunufaika na kazi zao baada ya kuuza kazi hizo nje ya nchi kupitia minada na njia nyingine ambapo kazi huuzwa kwa

bei za juu ilihali msanii kutokupata chochote  kutokana  na mauzo hayo zijulikanazo kama ‘resale royalties rights’.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw.Matiko Mniko alieleza kuwa Baraza katika kutatua changamoto ya Masoko kwa Wasanii wa Sanaa ya Ufundi wameanzisha Kampeni ambayo itashirikisha taasisi mbalimbali kuanzisha minada ambayo itakuwa ikifanyika Dodoma na Dar es Salaam angalau mara mbili kwa mwaka.

Mkutano huo uliratibiwa na BASATA chini ya Kaimu Mtendaji Matiko Mniko na kuhudhuriwa na Rais wa Shilikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Bibi m Doreen Sinare na mwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa (WHUSM) Bw.Habibi Msami.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com