METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 5, 2021

SAO HILL WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUWANUNULIA WANANCHI MICHE YA MITI

Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiwa  katika akishuhudia tukio la afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina akikabidhi miche ya miti kwa kiongozi wa kikosi cha JKT Mafinga
Baadhi ya wananchi na wadau wakikabidhiwa miche ya miti kutoka kwa uongzi wa shamba la miti la Sao Hill.
 
Na Fredy Mgunda,Iringa. 

ZAIDI ya miche ya miti milioni moja yenye gharama ya shilingi milioni 200 hugawiwa kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya misitu na kutunza uoto wa asali na wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa.

Akizungumza wakati kugawa miche hiyo kwa wananchi na wadau mbalimbli,Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema lengo la kutoa miche hiyo kuendelea kuchukua hatua madhubuti za ulinzi shirikishi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuondosha hatari zitokanazo na uharibifu wa mazingira

Alisema kuwa Jamii,Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma
yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya binadamu.

Alisema ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku akitaja za kutoweka kwa bayoanuai

Mwita alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.

Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.

“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema

Alisema upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.

Aidha Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.
 

Akizungumza kwa niaba mkuu wa wilaya ya Mufindi,afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina alisema kuwa kitendo cha viongozi wa shamba la Sao Hill kutoa miche ya miti milioni moja bure kwa wananchi wa wilaya hiyo ni kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla kutokana na faida za miti. 

Alisema kuwa uwepo wa shamba la miti katika shamba hilo la serikali limechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi wengine wa wilaya hiyo kuanza kupanda miti na hadi hii leo bado wanapanda miti na umekuwa uchumi wa wananchi. 

Mchina alisema kuwa kitendo cha kutoa miti hilo bure kunawakumbusha wananchi kuendelea kupanda miti kwenye mashamba yao ili kuendeleza utamaduni wa kupanda miti ili kukuza uchumi kwa wananchi wanaolizunguka samba hilo. 

 Aliwaomba wananchi wa wilaya ya Mufindi kuacha tabia ya kukata miti hovyo ili kuokoa mazingira ambayo ndio yamekuwa yanasababisha wananchi wanapata chakula,maji na kadharika hivyo wananchi wanapaswa kupanda miti kwa wingi kwa lengo la kutunza mazingira. 

“Ni vema tukaendelea kutunza miti ya asili na kuendelea kupanda miti kwa kitaalamu kwa kufuata maelezo kutoka kwa wataalam ili kupunguza uharibu unaosababishwa na sisi wenyewe kwani misitu ni mali na uhai vile vile” alisema 

Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kulinda mazingira na kukuza uchumi kwa wananchi na amewapongeza viongozi wa shamba la miti la Sao Hill kwa jitihada za kuendelea kutunza mazingira.

Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonukaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com