METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, February 13, 2021

Mganga Mkuu wa serikali ahamasisha mazoezi


Mapema leo Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameongoza mazoezi ya pamoja akiwa na Watumishi wenzake kutoka Wizara ya Afya Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na Wananchi wa Jiji la Dodoma. Mazoezi haya yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Aidha baada ya mazoezi, Mganga Mkuu amehamasisha Wananchi kufanya usafi kwa kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Viwanja vya Nyerere Square.

Akiongea katika matukio hayo, Prof. Makubi ametoa wito kwa Wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Vikevile amewataka Wananchi kuimarisha usafi wa mazingira ili  kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com