Rais wa kamati ya Olimpiki ya Brazil Carlos Arthur Nuzman akizungumza wakati wa ufunguzi
Michezo
ya Olympiki ya msimu wa kiangazi imeshafunguliwa rasmi mjini Rio Brazil.
Sherehe hizo zilianza kwa fashifashi na ngoma na mipangilio ya dansi
katika michezo ya kwanza kufanyika katika ardhi ya Amerika kusini.
Sherehe
za ufunguzi wa michezo ya olimpiki mjini Rio zilianza kwa fashifashi
pamoja na miondoko ya ngoma na dansi jukwaani jana Ijumaa wakati Brazil
ikijaribu kusahau miaka saba ya maandalizi yaliyokumbwa na matatizo
kadhaa na jamii ya wanaolimpiki wakijaribu kusahau kwa muda mzozo wa
wanamichezo kutumia madawa ya kuongeza nguvu misuli yaliyopigwa marufuku
yaani doping.
Wapenzi
wa michezo wapatao 78,000 walijazana katika uwanja maarufu wa Maracana
kuangalia tamasha hilo lililochukua muda wa saa nne ambapo wanamichezo
kama Michael Phelps pamoja na wanamichezo wengine nyota wakichukua
nafasi ya juu katika mashindano hayo ya kwanza ya olimpiki kufanyika
katika ardhi ya America kusini.
Mwimbaji
wa Brazil Paulinho da Viola aliimba wimbo wa taifa pamoja na watoto na
kuanzisha tamasha hilo lililopambwa kwa taa za rangi ngoma na dansi
kabla ya wanamichezo kufanya gwaride kwa kupita mbele ya watazamaji.
Kuvumiliana na heshima
Watayarishaji
wamesema sherehe ya ufunguzi ililenga katika kutuma ujumbe wa
kuvumiliana na kuheshimiana. Lakini imekuja wakati Brazil inapambana na
hali mbaya ya mdororo wa uchumi, idadi kubwa ya watu wasio na ajira na
ongezeko la uhalifu pamoja na mtafaruku wa kisiasa.
Wakati
muda ukikaribia wa kuanza kwa sherehe za ufunguzi, maelfu ya
waandamanaji waliingia mitaani kuonesha hasira zao kwa watawala nchini
Brazil na gharama za mabilioni ya dola kwa michezo hiyo.
Wakibeba
mabango yanayosema "Hapana kwa Olimpiki" , kiasi ya watu 3,000
walikusanyika nje ya hoteli ya kifahari ya Copacabana Palace , ambako
wanariadha wengi wanaoshiriki mashindano hayo ya olimpiki wanaishi.
Polisi walikuwa tayari lakini kuwatawanya waandamanaji kwa mabomu ya
kutoa machozi.
Mwenge wa olimpiki
Brazil
imetumia zaidi ya dola bilioni 10 kwa ajili ya miundo mbinu mipya na
matayarisho kwa ajili ya michezo hiyo katika wakati wa mzozo wa
kiuchumi. Sherehe hizo za ufunguzi zinaanzisha siku 17 za michezo mbali
mbali ilishirikisha kundi la wanamichezo maarufu ikiwa ni pamoja na
mfalme wa mbio fupi Usain Bolt na nyota katika kuogelea Michael Phelps
ambayo itakamilika ifikapo Agusti 21.
Na mwenge
wa Olimpiki uliingia mjini Rio kabla ya sherehe hizo, lakini gwiji wa
soka la Brazil Pele alisema hataweza kuubeba mwenge huo kutokana na hali
mbaya ya afya yake.
Idadi
kubwa ya wanajeshi na polisi wapatao 85,000, mara mbili kuliko
ilivyokuwa katika mashindano ya Olimpiki ya mjini London mwaka 2012,
watawekwa katika mji huo kuzuwia kitisho cha uhalifu wa mitaani na
mashambulizi ya kigaidi.
Hali hiyo hata hivyo haijaleta unafuu , kwani kumeshanza kutokea udokozi katika kijiji cha wanamichezo wa Olimpiki.
Ujumbe wa
wanamichezo kutoka Danmark, China na Australia wameripoti tayari vifaa
vyao kuibiwa. Waandishi habari wameibiwa kamera zao na laptop.
Medali 18
zitanyakuliwa katika siku ya kwanza rasmi ya michezo hiyo hii
leo.Ujumbe wa wanamichezo kutoka Danmark, China na Australia wameripoti
tayari vifaa vyao kuibiwa. Waandishi habari wameibiwa kamera zao na
laptop.
Medali 18 zitanyakuliwa katika siku ya kwanza rasmi ya michezo hiyo hii leo.DW
0 comments:
Post a Comment