METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, February 13, 2021

"JPM LIKIZO CHATO TU" DKT MWIGULU NCHEMBA


Na Mathias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria-Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba, amewaambia Watanzania kwamba wanayo bahati sana kuwa na Rais ambaye usiku na mchana anawaza namna ya kuwaletea maendeleo ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo marais wake hugeuza mahoteli kuwa ofisi zao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 13, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akizungumza kwa niaba ya waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

"Mimi nimezifuatilia sana hizi siasa na nilikuwa ninazipenda tangu nikiwa shule ya msingi, Afrika hapa kupata Rais ambaye masaa 24 kwa wiki, kwa mwaka mzima na kwa awamu nzima anashughulika na maisha ya watu wake tu ni ngumu kumpata, kuna marais wanaongoza nchi wakiwa hotelini na mke wake, wa kwetu akitaka likizo unamuona yuko Chato tu ana anaendelea kuchapa kazi", amesema Waziri Nchemba

Aidha akizungumzia kuhusu deni la Taifa, Waziri Nchemba amesema kuwa deni bado ni stahimilivu.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com