METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 28, 2021

Watoto Chini Ya Miaka 5 Hatarini Kupata Kichocho


Na Saleh Ramadhani

Kaimu Mganga Mkuu Wa Serikali Dokta Saitor Laiza amebainisha kuwa  Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano  na watu wenye umri wa kati wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maabukizi ya ugonjwa wa kichoho.

Hayo yameelezwa na Kaimu mganga mkuu wa serikali dokta  saitor laiza  katika mkutano na wadau wa afya uliokuwa na lengo la kufahamishana juu ya matokeo ya utafiti  ya ugonjwa wa kichocho uliofanywa  na NIMR katika kipindi cha miaka miwili

Kaimu mganga mkuu wa serikali Amesema matokeo yanaonyesha  kuwa baadhi ya maeneo hapa nchini bado yanachangamoto ya ugonjwa huo hasa maeneo yanayozunguka kanda ya ziwa  huku idadi kubwa ya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakiadhirika Zaidi.

"Ugonjwa wa kichocho bado ni changamoto kubwa katika maeneo ya ziwa victor,ziwa Nyasa na ziwa Tanganyika,idadi kubwa  ya watoto na watu wenye umri wa kati hadi miaka 55 waliopimwa katika Eneo la Ukerewe wameathirika katika sehemu kubwa na Tafiti kama hizi zinatuamsha sisi watekelezaji wa mifumo ya Afya na Matibabu" Amesema

Aidha amezishauri mamlaka zinazohusika ikiwemo tamisemi  kwakuwa wao wana mamlaka makubwa kufika katika maeneo yaliyoathirika kuona namna ya kusaidia kuwatibu ilikuokoa vifo vingi ambavyo vinaweza kutokea.

"Nizishauri Mamlaka husika kama ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ambao ndiyo watekelezaji wakubwa katika maeneo ambayo yanamadhara makubwa hata katika bajeti zetu tuzipange vizuri ili tuweze kuwaokoa watoto wasiende kuwa na madhara ya muda mrefu na pia tutaokoa vifo vingi" Amesema 

Naye Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti NIMR na mtafiti kiongozi wa mradi wa tiba Dokta Paul Kazyoba  ameeleza s kuwa waliamua kufanya utafiti juu ya ugonjwa huo baada ya kuna haupewi kipaombele kama magonjwa mengine na kubaini kuwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaathirika Zaidi hasa katika  wilaya za nyasa na ukerewe.

"Katika mkutano wetu tumeangalia ukubwa wa tatizo la kichocho kwa watoto umri chini ya miaka mitano,ni moja ya Tafiti ambazo zipo kwenye Mradi wa Tiba na Matokeo yake yapo Tayari kufanyiwa Kazi ili kuondoa Tatizo la kichocho nchini" Amesema kazyoba.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com