Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Thadei Luoga akifafanua jambo kuhusu kazi za kituo hicho. |
Mjumbe wa Bodi ya Mkurabita, Haji Janabi (katikati) akitoa ushauri jinsi ya kuboresha kituo hicho. Kulia ni Mratibu wa Mkurabita, Dkt. Seraphia Mgembe na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay.. |
Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mkurabita akiuliza swali kwa Afisa Biashara, George Mwaseba. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Eluminata Mwenda (katikati) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mkurabita walipowasili ofisini kwake . |
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya watendaji wa Mkurabita wakiwa ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Njombe Mji. |
Wajumbe wa Bodi na watendaji wa Mkurabita wakiondoka katika halmashauri hiyo baada ya kutembelea Kituo Jumuishi cha Biashara.
Njoolay akijadiliana jambo na Dkt. Mgembe walipokuwa wakiondoka baada ya kutembelea kituo jumuishi cha biashara.
Balozi mstaafu Njoolay akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Immaculate Senje pamoja na Dkt. Senje wakiondoka katika halmashauri hiyo kwendelea na ziara ya kikazi mkoni humo ambapo pamoja na mambo mengine walifanya kikao na wanufaika wa Mkurabita kwenye Ukumbi wa UWT mjini Njombe.
KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay imetembelea Kituo Jumuishi cha Biashara kilichopo Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Walipofika katika kituo hicho walielezwa na Afisa Biashara wa Halmashauri, George Mwaseba kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kituo hicho ambacho kimewezeshwa na Mkurabita samani na vitendea kazi vikiwemo kompyuta 3, scanner, Printer na meza ambavyo vimerahisisha kazi na kuifanya halmashauri kuongeza mapato kupitia malipo ya leseni za biashara.
Mwaseba amesema uwepo wa kituo hicho umewapunguzia usumbufu wananchi kwani sasa huduma karibu zote zinapatikana hapo.
0 comments:
Post a Comment