METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 29, 2021

ULEGA aagiza Serikali za mitaa kutobadilisha matumizi ya viwanja vya michezo

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akziungumza na walimu wa Shule ya Secondari Lusango iliyopo Turiani Wilaya ya Mvomero.Waziri Ulega amesisitiza michezo kupewa kipaumbele shuleni hapo ili kuibua vipaji.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akimkabidhi mipira kwa aijli ya maendeleo ya michezo Mkuu wa shule ya sekondari Lusango iliyopo Turiani Wilayani Mvomero Bi.Bahati Omary.


Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega ameagiza viongozi walioko Serikali za mitaa kutobadili matumizi ya viwanja vya michezo.


Waziri Ulega amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya michezo katika mkoa wa Morogoro.


“Viwanja vyote vilivyo katika ngazi ya vijiji viheshimiwe na vilindwe ili kuhakikisha vijana na watoto wanapata nafasi ya kucheza ili kuibua vipaji”aliongeza Ulega


Waziri Ulega amesema michezo ni afya,ajira,uchumi na inajenga undugu na Amani na utulivu.


Kwa upande mwingine Naibu waziri uyo amesema walimu wana jukumu Kubwa la kuvilinda viwanja vilivyoko katika maeneo yao.


“Nawaagiza walimu wawabane maafisa elimu waliopo katika maeneo yao katika ngazi za kata na wilaya kuhakikisha viwanja hivi vinalindwa ili kuhakikisha havitumiki kwa jambo lingine”amesisitiza Ulega


Katika hatua nyingine Naibu waziri Ulega ametoa mipira kwa shule ya msingi Manyinga na Shule za sekondari za Lusango na Morogoro zote zilizopo mkoa wa morogoro kwa ajili ya maendeleo ya michezo mkoani hapo.


Naibu Waziri Ulega alianza ziara yake katika mkoa wa Dodoma lengo kuu ikiwa kujua changamoto zilizopo katika michezo katika maeneo mbalimbali ili kuzifanyia kazi na kukuza michezo nchini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com