METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 27, 2021

EWURA KUFUTA BEI MPYA ZA MAJI

Na Saleh Ramadhani.

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za Nishati  na Maji nchini (EWURA)imetangaza kufuta bei zote mpya za maji ambazo zilitakiwa kuanza kutumika kuanzia Januari mwaka 2021 ambapo Mamlaka zote za Maji nchini zitaendelea kutumia bei za Mwaka 2018/2019.

Hatua hiyo ya EWURA imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko toka kwa wananchi kuhusu kubambikiziwa bei za Ankara na baadhi ya Mamlaka hizo ambapo kati ya malalamiko yote yaliyopokelewa ya umeme,mafuta na gesi asili  asilimia 60 yote ni ya maji.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Ankara za maji ambapo amesema hatua hiyo inaipa uwezo EWURA kufanya uchunguzi wa kina juu ya malalamiko hayo ya maji ili kubaini ukweli.

 "Jukumu la EWURA ni kupitia gharama na kuona kama zinauhalali kwa kulinganidha na gharama za kipindi cha nyuma za mamlaka husika pamoja na mahesabu ya fedha yaliyokaguliwa na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Gharama hizo hugawanywa kwa wateja wote kulingana na Matumizi yao ya Maji na Ndipo bei za maji kwa kila daraja la mteja hupatikana" Amesema.

Amesema kilio kikubwa kutoka kwa watekja wa huduma za maji kipo kwenye Ankara za maji ambapo asilimia 75 ya malalamiko yote kwenye maji ni malalamiko juu ya kutokubaliana na Ankara za maji zinzazotolewa na Mamlaka za Maji mbalimbali huku Malalamiko mengine ambayo ni makubwa ni migogoro ya uunganishaji huduma za maji ambayo ni asilimia 13.

Aidha amesema kuwa upangaji wa bei za Maji za Mamlaka za Maji na usafi wa mazingira hufanywa na EWURA kwakuzingatia Sheria ya EWURA namba 114 na Sheria ya Maji ya Mwaka2019 hivyo kwakuzingatia sheria hizo zipo kanuni za kupanga bei ambapo Mamlaka hiyo hupitia hatua kuu nne wakati wakufanya mchakato wa maombi ya mabadiliko ya bei yanayo wasilishwa kwake na Mamlaka za bei.

 "Hatua hii inachukuliwa ili kuipa uwezo EWURA kufanya uchunguzi wa kina juu ya malalamiko haya ya Maji ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo ambapo baada ya kumaliza shughuli ya uchunguzi wa kiufundi, EWURA itatoa maelekezo mengine ya Matumizi ya bei ambazo zilitakiwa kuanza January 2021" Amesema.

Pia amesema kuwa EWURA huanisha bei kwa Mamlaka za maji za miaka  mitatu ambazo bei nyingi ziliidhinishwa kwa Mwaka 2018/2019,2019/2020 na 2020/2021 ambazo zilikuwa zinaendelea kutumika.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com