Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar akinywa maji yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akiwa na wadau mbalimbali wanaokuwanywa maji hapoBalozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la maji ya kunywa la kiwanda cha Mkwawa wakati wa maonyesho ya kibiashara ya mkoani Iringa yaliyofanyika katika chuo cha Mkwawa balozi David Concar alisema kuwa amepongeza uzalishaji bora wa maji hayo ambayo yamekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa afya ya binadamu.
Balozi Concar alisema kuwa amekunywa maji hayo na kugundua kuwa yanaradha ya maji hayo ambayo anaamini kuwa kila mtu atayeonja maji hayo lazima avutiwe kwa namna yalivyokuwa bora.
Alisema kuwa amevutiwa na bidhaa hiyo ya maji ya kunywa ya kampuni ya Mkwawa na kuahidi kuitangaza kokote Kule atakapokuwa ametembea kutoka na kuvutiwa na jinsi ya uzalishwaji wake ulivyokuwa na bora wa kimataifa.
Balozi Concar aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho cha uzalishaji wa maji kuhakikisha wanatanua na kijitangaza zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ametembea kwenye super market nyingi hajaona maji ya kampuni hiyo ambayo yeye anaamni kuwa in maji bora hapa nchini.
Akiwa ameambatana na balozi wa uingereza nchini Tanzania, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa amekuwa balozi wa kujitegemea kuyatangaza maji hayo kila kona ya Tanzania kutokana na ubora wake.
Alisema kuwa anamuomba balozi huyo Nate awe balozi wa kutangaza maji yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kutokana na ubora wake ambao maji hayo yanayo.
Kasesela aliwataka viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatanua wigo wa masoko ya bidhaa hiyo ya maji ya kampuni ya uzalishaji wa maji ya Mkwawa inayopatikana mkoani Iringa wilaya ya Iringa.
Alisisitiza wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kuendelea kunywa maji safi na salama yanayozalishwa na kiwanda cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa kutokana na ubora wake.
Kwa upande wao baadhi ya wanachi mkoani Iringa waliohudhulia katika maonyesho hayo yaliyofanyikia katika chuo cha Mkwawa waliyapongeza maji hayo safi na salama kwa kunywa kutokana na ubora wake.
Walisisistiza kuwa wataendelea kunywa maji hayo yaliyokuwa na ubora wa hali ya juu lakini wanatakiwa kuhakikisha wanaulinda na kuuboresha ubora wake ambao upo hadi hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment