Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Juliana Chipanjilo Mtumishi wa Wizara ya Kilimo nyuma ya Waziri ni Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020 wakati ambapo Mawaziri hao walipokelewa rasmi Wizarani baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 9 Desemba, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma; Tangu wakati huo walianza mara moja kutekeleza majukumu yao katika mikoa tofauti.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakijadiliana jambo kwa mara ya kwanza katika Ofisi ya Waziri katika majengo ya Wizara ya Kilimo Mtumba Mji wa Serikali mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020. Mawaziri hao waliapiashwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 9 Desemba, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Tangu wakati huo walianza mara moja kutekeleza majukumu yao katika mikoa tofauti.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilmo Gerald Kusaya akisoma taarifa maalum ya Wizara wakati wa hafla ya kuwakaribisha rasmi Wizara ya Kilimo; Waziri Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu wake Mhe.Hussein Bashe mchana wa leo tarehe 21 Desemba, 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakifuatilia utambulisho kutoka kwa Wakuu wa idara/ Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo leo tarehe 21 Desemba, 2020 mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara Mtumba Mji wa Serikali.
Waziri
wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo mchana tarehe 21 Desemba, 2020
amepokelewa rasmi Wizara ya Kilimo katika Ofisi za Wizara hiyo katika Mji wa
Serikali Mtumba na kutoa wito kwa Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa
Taasisi kufikia kuongeza tija kwenye Sekta ya Kilimo Mazao hususan zao la ngano
na mazao mengine ya biashara.
Waziri
wa Kilimo Prof. Mkenda ambaye aliambatana na Msaidizi wake; Naibu Waziri Kilimo
Mhe. Hussein Bashe wote kwa pamoja leo wamepokelewa rasmi na Watumishi wa
Wizara ya Kilimo katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma na wote kwa pamoja
wamesisitiza na kuomba ushirikiano ili kuifaya Wizara ya Kilimo kuongeza tija
kwenye mazao ya kilimo.
Katika
hafla hiyo ya mapokezi wote kwa pamoja; Walipata nafasi ya kuongea na
Menejimenti ya Wizara ambapo Waziri Mkenda amesema Wizara inajukumu kubwa la
kuhakikisha taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula pamoja na kufanya Sekta
ya Kilimo Mazao inachangia mara dufu katika pato la taifa.
Waziri
Mkenda ameongeza kuwa tija kwenye kilimo bado ipo chini na kuongeza kuwa mazao
yanachangia asilimia 18 ya pato la taifa wakati Sekta ya Kilimo kwa ujumla
inachangia takribani asilimia 28.2 ya pato la taifa, asilimia 58 ya ajira na
asilimia 65.5 ya malighafi inayotumika katika Sekta ya Viwanda, asilimia 28.2
ya pato la taifa na asilimia 30 ya mapato ya fedha za kigeni.
“Ukiangalia
zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wameajiriwa kwenye Sekta ya Kilimo; Jambo
hili ni lazima tulifanyie kazi kwa ukaribu na kuleta mapinduzi ya kweli. Nchi
zilizoendelea unakuta asilimia tano tu (5%) ndiyo wameajiliwa maana yake ni
kuwa tija ipo chini, unatakiwa kuwa na idadi ndogo na wengine wajikite kwenye
Sekta nyingine”. Amesisitiza Waziri Mkenda.
Naye Naibu Waziri Bashe amesema ili Wizara ifikie malengo yalikusudiwa ni vyema Viongozi pamoja na Watumishi wote wa Wizara kubadili fikra.
0 comments:
Post a Comment