Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy
Mwalimu akiteta jambo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Ikulu Zanzibar. Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa lengo la
kujitambulisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Mwalimu hii leo amefanya ziara ya kikazi
visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.
Waziri Ummy amekutana na kufanya mazungumzo
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi Ikulu Zanzibar. Katika mazungumzo yao Mhe. Mwalimu amesema kwa
kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar amedhamiria
kuendeleza jitihada za kutatua changamoto za Muungano zilizobakia.
“Mhe. Rais nikuhakikishie kuwa nitafanya
kazi kwa karibu sana na Mhe. Khalid Waziri mwenzangu kuhakikisha hoja ambazo
bado hazijapatiwa ufumbuzi zinafanyiwa kazi na mwanzoni mwa mwezi Januari
tunategemea kuwa na kikao cha pamoja baina yetu” Alisisitiza Mhe. Ummy.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mhe.
Ummy Mwalimu wa kuteuliwa tena kuwa Waziri na kusisitiza kuwa Serikali yake
itampa ushirikiano katika kuratibu masuala ya Muungano.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy Mwalimu
amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad
Chukwani Zanzibar.
Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara
zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na
kuhamasisha Wizara zisizo na hoja
kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.
“Nashauri na kusisitiza Wizara
zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe
ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.
Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.
0 comments:
Post a Comment