Hayo ameyasema
hii leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa eneo la mradi
wa upandaji miti na kuhifadhi mazingira
katika eneo la medeli lenye ukubwa wa
hekta 9 ambapo takribani miti 4,330 imepandwa katika eneo hilo.
Amesema, jitihada zilizofanywa na kampuni ya Vodacom na WWF ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kutekeleza azma ya agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alilolitoa mwaka 2017 katika uzinduzi wa kampeni ya Kijanisha Dodoma.
“Kuna uhitaji mkubwa wa kuboresha Mazingira ya mkoa wa Dodoma kwa kuotesha miti kwa wingi; kuhakikisha inakua na kuhifadhi Mazingira yetu, hivyo nitoe rai kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maliasili na Utalii, Asasi za Kiraia, sekta binafsi na washirika wa maendeleo kutathmini utekelezaji wa mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016 -2021” alisisitiza Mhe. Ummy.
Amesema ili
kampeni ya kijanisha Dodoma ifanikiwe ni jukumu la kila mwana Dodoma na
wadau kupanda miti kwenye maeneo
mbalimbali kwa lengo la kuboresha Mazingira ya Dodoma.
“Kwa kuwa niña dhamana ya Kusimamia masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira, nitoe pongezi za dhati kwa Kampuni ya Vodacom; WWF na Jiji la Dodoma kwa juhudi mlizoonesha katika kusimamia utekelezaji wa mradi huu wa upandaji miti ambao ni muhimu kwa ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho” Mhe. Ummy alisisitiza.
Kwa upande
mwingine Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe ametoa rai kwa
watanzania kubadili dhana ya kupanda miti na kuwa kuamua kustawisha miti huku
akitoa rai ya kuanzishwa kwa mashindano ya upandaji miti mashuleni.
Kampuni ya simu
ya Vodacom kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) na Jiji
la Dodoma wameuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na athari za
mabadiliko ya Tabianchi kwa kutekeleza mradi wa upandaji miti katika eneo la
Medeli na maeneo mengine Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment