METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 11, 2020

UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE KWENYE MRADI WA STAMICO LAZIMA UANZE-WAZIRI BITEKO

Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Wizara ya Madini kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal)

Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Madini wakifuatilia kikao kazi kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020.

Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Wizara ya Madini kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Prof Shukrani Manya akizungumza wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara ya Madini kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila akizungumza wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara ya Madini kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020. Wengine pichani ni Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko (Katikati) na Naibu Waziri wa Madini Mhe Prof Shukrani Manya (Kulia)

Na Mathias Canal, Wazo Huru-Dodoma

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko ameeleza mpango huo wa serikali wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wote wa Wizara hiyo kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020.

Katika kikao kazi hicho kilichochagizwa na mapokezi ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Prof Shukrani Manya, Waziri Biteko amebainisha kuwa changamoto na mvutano uliopo baina ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unapaswa kufika ukomo ili shughuli za uchimbaji makaa ya mawe uweze kusonga mbele.

Amesema kuwa viongozi wote wa Wizara ya Madini wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha dhamira hiyo ya serikali kwa maslahi makubwa na manufaa ya wananchi.

“Tutakuwa na urafiki mahali tutakapokuwa tunafanya vizuri na kununiana pale ambapo hatutafanya vizuri na mimi kiu yangu ni kuona wote tunafanikiwa” Amesema Biteko

Awali Waziri Biteko amewaasa watendaji wa Wizara hiyo ya Madini kubadilika kutokana na mazingira kwani mazoea waliyokuwa nayo kabla ya uteuzi wa Naibu Waziri yanapaswa kumalizika na kulinda heshima ya viongozi hao.

“Mazoea sio mahala pake kwa sasa, na mkiona Mhe Rais amemteua kiongozi kutoka kwenye Wizara ya Madini maana yake ameona utendaji uliotukaka kwani ana watanzania wengi wenye uwezo wa kufanya kazi kwa weledi lakini wakati mwingine anatoa upendeleo” Amekaririwa Mhe Biteko

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Mhe Prof Shukrani Manya amesema kuwa matokeo mazuri ya ufanyaji kazi wa watendaji wa Wizara ya Madini ndio umempatia ngazi ya kupanda daraja hivyo amewataka kuongeza bidii na ufanisi katika kazi ili kufikia adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Mhe Manya amewasisitiza watumishi wote kuendeleza ushirikiano ili kufikia dhamira ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 pamoja na mikakati madhubuti ambayo wizara na taasisi zake imejiwekea.

MWISHO

Share:

3 comments:

  1. Hongera sana wizara ya madini kwa mikakati mizuri yenye tija hakika watanzania tuko tayari kutoa ushirikiano wetu kwenu ili kuinua uchumi wa nchi yetu. MADINI YETU UCHUMI WETU.

    ReplyDelete
  2. Nimeona Dhamira ya kweli ya serikali yangu Hasa kwenye kufufua mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwila na Kuanzisha Migodi mingine mingi ndani ya Tanzania

    ReplyDelete
  3. Tunawashukuru kwa mipango mizuri nategemea mgod wa mchuchuma nao utaanza kazi maana miaka mingi toka nikiwa mdogo hadi sasa naendea uzee ni
    hadithi tuu

    ReplyDelete

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com