METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 18, 2020

RC KUNENGE AWAPA SIKU TATU DAWASA KUHAKIKISHA WANAFIKISHA HUDUMA YA MAJI SAFI KWA WAKAZI WA MTAA WA MPAKANI KATA YA KWEMBE


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa siku tatu kwa DAWASA kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuunganisha Bomba kubwa la Maji na kufikisha huduma ya Maji safi wakazi wa mtaa wa Mpakani kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo.

RC Kunenge ametoa agizo hilo wakati alipowatembelea wakazi hao baada ya kupaza sauti zao juu ya ukosefu wa Maji safi na Salama ambapo amesema baada ya kukamilisha zoezi la kuunganisha Bomba kubwa na kufikisha maji kwa wananchi ambao tayari wamewekewa miundombinu ya mabomba wahakikishe wanafanya pia utaratibu wa kufikisha huduma hiyo na kwa wale ambao bado hawajawekewa miundombinu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema wamejipanga kufanya kazi kwa juhudi zote ili kuhakikisha ifikapo Jumapil agizo la Mkuu wa Mkoa linakuwa limetekelezwa kwa asilimia mia moja na kwa ufanisi mkubwa.

Nao wakazi wa eneo hilo la Kwembe wamemshukuru RC Kunenge kwa kusikia kilio Chao na kuamua kufunga safari kwenda kuwasalimia Jambo na wanaamini maagizo aliyotoa yatatekelezwa na Mamlaka husika.

Aidha Wakazi hao wamesema kitendo Cha RC Kunenge kusikia kilio Chao na kwenda kuwatembelea ndani ya muda mfupi kinaonyesha namna Serikali yao inawajali.  

Katika ziara hiyo RC Kunenge aliambatana pia na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Katibu tawala wa Manispaa hiyoo, Waandisi pamoja na Watendaji kutoka DAWASA.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com