METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 9, 2020

RC KUNENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA KISASA CHA NYAMA KIBAHA KUPATA UZOEFU WA KUENDESHA MACHINJIO YA VINGUNGUTI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametembelea kiwanda Cha kisasa Cha Uchinjaji na usindikaji wa Nyama Cha Tan Choice kilichopo  Soga Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu utakaotumika kuboresha machinjio ya kisasa Vingunguti.

Katika ziara hiyo RC Kunenge ameambatana na Watendaji kutoka Manispaa ya Ilala, Mkurugenzi wa NHC na Watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kujionea hatua zote za uchinjaji wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo kuanzia hatua ya Kwanza Hadi ya mwisho.

Akizungumza Katika ziara hiyo RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na namna kiwanda hicho kinazalisha nyama kwa viwango vya kimataifa jambo linalopelekea 80% ya nyama inayozalishwa Kiwandani hapo kuuzwa nje ya nchi.

Aidha RC Kunenge amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutafsiri kwa Vitendo ndoto ya Rais Dkt. John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda jambo lililowezesha kutoa ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Hata hivyo RC Kunenge amesema kiwanda hicho pia kitasaidia wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini kupata soko la uhakika la kuuza mifugo yao kwa Bei yenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Rashid Abdilah amesema kwa Sasa kiasi kikubwa Cha nyama nayozalisha wanaiuza kwenye mataifa ya Falme za kiarabu Kama Oman, Quatar na Kuwait na kueleza kuwa mahitaji ya nyama nje ya nchi bado ni makubwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com