Na Joyce Kasiki,Dodoma
HALMASHAURI ya jiji la Dodoma imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za lishe ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vituo vyote vya afya ya mama na mtoto/kliniki vinatoa elimu hiyo kwa lengo la kukabilina na udumavu jijini hump.
Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jijini dodoma, Mganga Mkuu wa jiji la Dodoma Dkt.Gatete Mahava alisema,moja ya mambo ambayo wamekuwa wakilifuatilia ni pamoja na katika vituo hivyo ambavyo vinaangalia kwa ujumla afya za akina mama wajawazito na watoto.
Alisema baadhi ya vituo ambavyo vilionekana kama vililegalega katika utoaji wa elimu hiyo ambavyo wameendelea kuvifuatilia na kuhakikisha vinatoa elimu ya lishe kwanakina mama wajawazito na wenye watoto walio chini ya umri wa miaka mitano .
Miongoni mwa vituo ambavyo vilionekana kutofanya vizuri na kuhojiwa na waandishi wa habari kuhusu suala hilo ni pamoja na kituo cha afya cha kwa Habiba ambacho baadhi ya akina mama walihojiwa na kisema kuwa hawajawahi kupata elimu ya lishe katika kituo hicho.
Dkt.Mahava alisema,kituo hicho sasa kinafanya vizuri na kitoa elimu kulingana na ratiba ambayo wamejiwekea.”alisema Dkt.Mahava
Hata hivyo alisema,utoaji wa elimu ya lishe katika vituo vya afya ya mama na mtoto hutolewa kwa mujibu wa ratiba iliyojiwekea kituo husika kulingana na watumishi wa afya waliopo katika kituo husika.
‘Upo mpango mkakati wa utoaji elimu ya lishe ili kuboresha afua ya lishe ambayo inaunganisha sekta zote katika kuboresha masuala ya lishe na moja ya kazi ambazo zimekuwa zikitekelezwa ni pamoja na kutoa elimu klini lakini,
“Pia kutengeneza mashamba darasa ya kutengeneza vyakula na kutoa elimu kwa akina mama na wajasiriamali wenye viwanda vidogo kwa ajili ya kutengeneza vyakula kwa mfano wenye mashine za kusaga unga wanaelekezwa namna gani kuweka madini katika vyakula hivyo .”alisema Dkt.Mahava vile vile alisema,wameendelea kupita maeneo mbalimbali kuhakikisha wanaovuna chumvi,wanaweka madini ya iodine.’alisisitiza
Kwa mujibu wa Dkt.Mahava ,Idara ya afya upande wa lishe imeendelea kusimamia utoaji wa elimu na kufundisha katika utendaji wa kazi lakini pia kutoa dawa na kuhakikisha wanakagua vyakula vya watoto vinavyouzwa madukani ili kuhakikisha vimewekwa virutubisho vinavyohitajika.
0 comments:
Post a Comment