METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 16, 2020

JUMLA YA VIJANA 2000 KUTOKA MKOA WA IRINGA KUFIKIWA NA MRADI WA LYRA IN AFRCA

Msimamizi wa mradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue akitoa elimu kwa baadhi ya vijana waliopo kwenye mradi huo
Msimamizi wa maradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue akitoa elimu kwa baadhi ya vijana waliopo kwenye mradi huo
Baadhi ya vijana washiriki wa mafunzo yanayotolewa na
maradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA. 

 Na Fredy Mgunda,Iringa

JUMLA ya vijana 2000 kutoka kwenye wilaya tatu za mkoa wa Iringa kufikiwa na mradi wa imarika kijana wa LYRA IN AFRCA  wenye lengo la kufungua fikra na mitazamo chanya kwa vijana katika Maisha yao. 

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa baadhi ya vijana ambao wapo kwenye mradi huo, msimamizi wa mradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha vijana kutambua fursa zilizopo na kuzifanyika kazi kwa kupata matokeo chanya.

Alisema kuwa mradi huo unafadhiliwa na watu wa uingereza kwa kuwezesha kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana ambao watakuwa wanatoa elimu kwa vijana na watu wengine kutoka kwenye jamiii ambayo wanaishi huko vijijini kwao.

Mafue alisema kuwa wameshafanikiwa kufanya mafunzo kwa vijana wa vijiji kumi na moja kutoka katika wilaya ya Iringa na Kilolo ambopo hadi sasa takribani vijana 401 wameshafikiwa katika awamu ya kwanza wakitegemea kuanza awamu ya pili mwaka 2021 mwezi wa pili kwa lengo la kufikia vijana wote waliolengwa na mradi.

Alisema kuwa lengo kuu mradi huo ni kuwawezesha vijana kuzitambua fursa zilizopo katika maeneo wanaishi na kuzigeuza kuwa fursa kiuchumi na kukuza maendeleo na kusaidia vijana wasikimbilie mijini na kuzitelekeza fursa zilizopo vijijini.

Mafue alisema kuwa mradi huo unahusisha vijana wenye umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nane ikiwajumisha vijana walemavu na mzazi mmoja ambao hawana fursa yoyote na kuwasaidia kisaikolojia kuanza kuzichangamkia furs ana kujikombo kimaisha.

“Tunawasaidia pia mzazi mmoja ambaye alipata mimba akiwa shuleni au akiwa na umri mdogo kuzitambua furs ana kuzitumia ili kujikomboa kiuchumi na matumaini kwa vijana wanaoishi vijijini yameongezeka kwa vijana hao kuanza kufanya biashara za kiuchumi” alisema Mafue 

Alisema kuwa mafunzo ya imarika vijana yamesaidia uundwaji wa vikundi vya kiuchumi ambapo hadi sasa jumla ya vikundi 21 tayari vimeundwa na vinafanya vizuri katika kukopa na kukopesha kwa lengo la kuinua kiuchumi.

Shuhudia Chang’a anatokea Kijiji cha Imalutwa alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na faida ya kusaidia kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya kiuchumi tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupata mafunzo kutoka LYRA IN AFRICA.

Naye Yasinta Migodela alisema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kuboresha ufanisi wa kibiasha kwa kuwa hapo awali alikuwa anafanya biasha bila ya kuwa na mafunzo na kumpelekea kupata hasara lakini baada ya kupata mafunzo yamsaidia jinsi ya utunzaji wa fedha na mpangilio mzima wa biashara.

Kwa upande wao Stanslaus Mtweve,Nestory Simagunga,Cassian Kihongosi na Rebeka Mbwilo walisema kuwa mafunzo waliyopata kutoka katika shirika la LYRA IN AFRICA yamewasidia kuwakomboa kiuchumi na kifikra kutokana na elimu waliyopewa. 

“Mara baada ya kupewa mafunzo hayo na shirika la LYRA IN AFRCA yalitusaidia kuridi katika vijiji vyetu na kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu ambao kwa asilimia furani tumesaidia vijana wengi kuacha tabia ya ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya na wameanza kujikita katika shughuli za kiuchumi ambazo kwa sasa zinachochea uchumi kukua” walisema.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com