Kufuatia uwepo wa Changamoto mbali zinazohusu Umeme Maeneo mengi hapa Nchini, Naibu Waziri wa Nishati Adv. Stephen Byabato (Mb) ametoa mwelekeo wa Wizara husika katika kutafutia Ufumbuzi Kero sugu za Umeme zinazowakabili Wananchi ambao kipekee ndio Watumiaji wa Nishati hiyo.
Naibu Waziri Byabato ambaye yupo Mkoani Kagera kwa Ziara ya Kikazi, ameoneshwa kusikitishwa na Kero ndogo ndogo zinazoendelea kuwakumba Wateja na Watumiaji wa Umeme, ambazo Ni Ukosefu wa Mita, Nyaya, Nguzo na wakati mwingine Uzembe, sababu ambazo zimeainishwa na Wananchi kutoka Maeneo mbalimbali Mkoani Kagera wakati wakitoa Kero zao, katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Desemba 22, 2020.
Miradi yote ya Umeme inayotekelezwa Nchini, hasa maeneo ya Visiwani na sehemu ambazo Umeme haujawafikia Wananchi, kuhakikisha Shirika la Umeme hapa Nchini TANESCO kuhakikisha wanasimamia Gharama za uuzaji wa Umeme huo kwa Wananchi, kulingana na Maelekezo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani Juu ya punguzo la Umeme huo, kwani maeneo mengine wamekuwa wakiuziwa Umeme zaidi ya Shilingi 100 kwa Unit moja.
Katika suala la wale ambao wameomba kuunganishiwa Umeme na bado hawajaunganishiwa kwa sababu mbalimbali na kupelekea suala Hilo kuchukua Muda Mrefu, Mhe. Byabato ameagiza TANESCO kutumia muda wa Siku Saba tu kukamilisha Mchakato wa Upembuzi na Tathimini ikiwa ni pamoja na Vipimo, kuanzia siku mteja akiomba Huduma hiyo, Kisha baada ya hapo Mteja akalipie gharama ya uunganishwaji Umeme kwa Shilingi 27,000/= Ndani ya Siku Tisini, na kuongeza kuwa wale wote ambao wameomba kuunganishiwa Huduma hiyo Ndani ya Mkoa Kagera wawe wameunganishiwa Huduma ya Umeme kufikia Tarehe 31 Januari 2021.
0 comments:
Post a Comment