METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, November 8, 2020

KUSHUKA KWA VIWANGO VYA WACHEZAJI KIPINDI CHA CORONA KULICHANGIA KUSHUKA DARAJA KWA TIMU YA LIPULI

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Lipuli iliyoshuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza ligi daraja la kwanza

Na Fredy Mgunda,Iringa.
 

UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Lipuli ya mkoani Iringa umesema kuwa kushuka daraja kutoka ligi kuu Tanzania Bara hadi ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kuna changiwa na mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona. 

Akizungumza na blog hii katibu wa timu hiyo ya Lipuli Jullias Leo alisema kuwa sababu za kushuka daraja inatokana na kulipuka kwa ugonjwa wa Corona ambao ulisababisha kusimama kwa ligi kuu Tanzania Bara na ligi nyingine nyingi duniani. 

Alisema kuwa baada ya Corona wachezaji wengi walirudi wakiwa wameongezeka uzito kutokana na wachezaji wengi kutofanya mazoezi kwa wakati kutokana mpangilio maalum wa kocha wa timu.

Leo aliongeza kuwa baada ya Corona timu hiyo ilishuka kiuchumi kutokana na wachangiaji wengi wa timu hiyo kushuka kiuchumi kutokana na Corona na kusababisha kusuka kwa uchangiaji wa fedha kwa wadau mbalimbali wa timu hiyo. 

Alisema baada ya Corona wachezaji muhimu wa timu hiyo kushindwa kurejea kambini kwenye timu hiyo kwa kuwa walikuwa Wanamadai ya fedha ambayo yalishindwa kulipwa kutokana timu hiyo kushuka kiuchumi. 

Leo alisema kuwa kutokana na sababu za Corona kocha wa timu hiyo ya Lipuli na baadhi ya wachezaji walishindwa kurejea kambini kwenye timu hivyo kupelekea kuathiri mfumo wa uchezaji wa timu kwa kuwa ili walazimu kutafuta kocha mwingine. 

"Unapozungumzia mchezaji kama Poul Nonga ndio alikuwa mfungaji bora wa timu yetu ya Lipuli hivyo baada ya Corona timu ilikosa huduma ya mchezaji muhimu hivyo timu ilikuwa inashindwa namna ya kufunga magoli mengi ambayo yangeisaidia timu yetu kubaki ligi Tanzania Bara"alisema Leo. 

Nao baadhi  ya wadau wa mpira  wa miguu mkoani Iringa Toshack Eliuter na Wiston kalumba walisema kuwa kutokana na Corona uchumi kwa baadhi ya wapenda michezo washuka kiuchumi na kusababisha kushindwa kuichangia timu na timu kushindwa kujiendesha yenyewe.  

Lakini pia waliongeza kuwa viongozi wa timu ya Lipuli walishindwa kuandaa maandalizi mazuri ya timu hiyo na kusababisha kuondoa kabisa mshikamano wa viongozi wa timu hiyo hadi pale zilipobakia mechi tano za mwisho ndipo wakarudisha mshikamano wao lakini walikuwa wamechelewa na kupelekea timu kushuka daraja kutoka ligi kuu Tanzania Bara hadi ligi daraja la kwanza Tanzania Bara. 

Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa timu ya Costal Union inashiriki ligi kuu Tanzania Bara  Hassan Ussi alisema kuwa kutokana na Corona wachezaji wengi walishuka viwango na kushindwa kufikia pale walipokuwa awali na kusababisha timu kama ya lipuli kushuka daraja kutoka ligi kuu Tanzania Bara hadi ligi daraja la kwanza.  

Alisema kuwa kutokana na Corona uchumi kwa timu husika ulishuka na kupelekea timu kushindwa kutoa huduma bora kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu husika hivyo timu ambazo havina vyanzo muhimu vya uchumi viliteteleka na kupelekea kushuka daraja. 

Ussi alisema kuwa ili timu ifanye vizuri kwenye mashindano lazima wachezaji wafanye mazoezi ya pamoja ili kutengeneza uelewano wawapo uwanjani kwenye mechi za kishindani na kupata matokeo mazuri. 

Naye daktari wa timu hiyo  Dr  Mwasabite alisema kuwa mchezaji akiongezaka uzito lazima atapata majeraha ya mara kwa mara kutokana na kutofanya mazoezi na baada ya janga la Corona  lilipelekea wachezaji wengi kushindwa kurudi kwenye viwango vyao kwa sababu ya kuongezaka uzito.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com