Katibu wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu Milton Lupa akizungumza jambo wakati wa kikao cha kawaida cha Bodi ya Ushauri ya NFRA kilichofanyika katika eneo la Maisaka Mjini Babati katika Mkoa wa Manyara, tarehe 25 Novemba 2020.
Na Mathias Canal, NFRA-Manyara
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA Leo tarehe 25 Novemba 2020 imekutana Mjini Babati katika Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kikao chake cha kawaida.
Katika kikao kazi hicho Bodi ya Ushauri imejadili Taarifa iliyowasilishwa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala ya mwaka wa fedha 2019/2020 pamoja na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za wakala wa Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Akizungumza wakati wa kikao hicho mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Yustas Kangole ameelezwa kuridhishwa na hatua zilizofikiwa ya ujenzi.
Pamoja na kueleza kuridhishwa huko, Mhandisi Kangole amebainisha kuwa yapo maeneo ambayo yanapaswa kufanyiwa maboresho ya haraka kabla ya kukabidhiwa kwa mradi huo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Milton Lupa amebainisha kuwa ujenzi wa vihenge vya kisasa pamoja na maghala mawili ya kisasa Wilayani Babati utaifanya NFRA kanda ya Arusha inayohudumu mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro kuongeza akiba ya Taifa ya Chakula kutoka Tani 39,000 hadi Tani 79,000.
Ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo unatekelezwa kwenye viwanja vya NFRA eneo la Maisaka ambapo ulianza rasmi Disemba 2018 na unatekelezwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka serikali ya Poland.
Naye, Meneja wa Uwekezaji na Usimamizi wa Milki wa NFRA ambaye ndiye mratibu wa Mradi huo Mhandisi Imani Nzobonaliba amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa nane ya Tanzania bara ikiwemo mkoa wa Manyara ambapo kanda ya Arusha kupitia mradi wa kuongeza uwezo wa Kuhifadhi nafaka unaendelea na ujenzi mpya wa vihenge nane vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 25,000 na maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 15,000
Ameosema kuwa kwa upande wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Kanda ya Arusha mradi huo umefikia Asilimia 97 huku kwa ujenzi wa mradi huo kwa nchi nzima umefikia Asilimia 78.7
MWISHO
0 comments:
Post a Comment