METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 18, 2020

MILIONI 177 KUKAMILISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU BUSWELU

Kiasi cha shilingi milioni mia moja na kumi na saba kinatarajiwa kutumika kwaajili ya kuhakikisha miundombinu ya elimu inakamilika ndani ya kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela ili watoto wa kata hiyo waweze kupata elimu iliyobora katika mazingira mazuri.

Hayo yamebainishwa na mgombea wa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akihutubia wananchi wa kata hiyo ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni uliofanyika katika viwanja vya Zembwela ambapo amesema kuwa katika mwaka mpya wa fedha wa 2020/2021 Serikali imetenga kiasi hicho Cha fedha kujenga miundombinu ya shule za Buswelu shule ya msingi, Bulola shule ya msingi na Bujingwa sekondari ili watoto wanaosoma shule hizo waweze kupata elimu bila changamoto yeyote ikiwemo kuwaepusha na tatizo la mimba za utotoni

'.. Tunaenda kuboresha miundombinu ili watoto wetu wasome vizuri pamoja na kuwaepusha watoto wa kike na mimba mitaani ..' Alisema

Aidha mgombea huyo Dkt Mabula akaongeza kuwa Ilani ya CCM inazungumzia ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo uimarishaji wa mfuko wa barabara pamoja na Ujenzi wa barabara ya kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kupitia Kayenze yenye urefu wa Kilomita 46 inayotamkwa ukurasa wa 76 wa Ilani ya Chama hicho kwa awamu ya 2020-2025 hivyo kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua tena pamoja na mgombea urais Dkt John Magufuli na diwani wa CCM kwa kata hiyo ili wakayatekeleze yaliyoahidiwa .

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akasisitiza wananchi hao juu ya umakini wakati wa zoezi la kupiga Kura ili kura zao zisiharibike sanjari na kuwaomba kuwapuuza wale wote wenye nia ovu ya kupotosha wananchi kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekwishashinda hivyo hakuna sababu ya kujitokeza kupiga kura.

Akihitimisha meneja kampeni wa CCM kwa Jimbo la Ilemela Ndugu Kazungu Safari Idebe akawataka wananchi hao kuchagua mgombea urais kutoka CCM, Ubunge na Udiwani ili ikawe rahisi kutekeleza shughuli za maendeleo sanjari na kuwambusha Jimbo hilo lilivyosimama katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakati wa utawala wa upinzani na miradi lukuki iliyotekelezwa katika Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli Mbunge akiwa Dkt Angeline Mabula hivyo kuwaasa kutojaribu tena kuchagua wagombea wa vyama pinzani kwani kufanya hvyo ni kuyakataa maendeleo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com