MHE BASHUNGWA AWATOA HOFU
WAFANYABIASHARA KUHUSU UBORA WA KOROSHO
Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe Innocent Bashungwa yupo ziarani katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma,
Pwani na Dar es salaam ili kujionea mwenendo wa hali ya ubora wa zao la korosho
kwenye maghala.
Mhe Bashungwa amesema kuwa
kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi katika maeneo mengi kuhusu ubora wa
korosho kuwa mbovu jambo ambalo halina ukweli. “Nilikuwa nikisikia na kutumiwa ujumbe na watu mbalimbali kuwa
korosho zilizonunuliwa na Serikali ni mbovu hivyo nimelazimika kufunga safari
ili kutembelea maghala ambayo yamehifadhi korosho ili kubaini ukweli uliopo.
Jambo muhimu kwa sasa
tunatafuta masoko kwa ajili ya kuziuza korosho zote” Alikaririwa Mhe Bashungwa.
Alisema kuwa, hali ya ubora wa korosho ilisababishwa na habari za uongo
zilizopo mitaani kuwa hazina ubora. Kwa maghala niliyopita kujionea na hali
ya korosho ipo katika hali nzuri.
Aidha, Waziri huyo wa viwanda
na Biashara amewasihi wafanyabiashara mbalimbali kujitokeza kuchangamkia fursa
ya ununuzi wa korosho hizo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment