Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wadau wa michezo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya cha jijini Dar es salaam kitakachosaidia kuwaandaa na kuongeza idadi ya wataalamu wa michezo nchini.Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuzindua Kituo cha Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Malya jijini Dar es salaam ambacho kitakachosaidia kuongeza idadi ya wataalamu wa michezo nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
amezindua kituo cha michezo ili kuwaandaa na kuongeza idadi ya wataalamu wa
michezo nchini.
Kituo hicho kinachoendeshwa na
cha Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kipo jijini Dar es salaam katika Uwanja
wa Benjamin Mkapa ambapo Dkt. Abbasi alibainisha kuwa kati ya mambo ambayo
alikuwa anajifunza baada ya kukabidhiwa wizara hiyo ilikuwa ni pamoja na
uendeshaji wa shughuli za Wizara na taasisi zake hatua iliyompelekea kuagiza
chuo hicho kiboreshwe ili iwe fursa ya kutengeneza wataalamu wa michezo wengi
nchini.
“Tumefanya uamuzi mgumu na muhimu
sana wa kuleta kituo cha chuo chetu cha Michezo Malya hapa Dar es salaam ili
kutoa na kuendeleza elimu ya michezo katika kada zote nchini na tunaamini
mahitaji ni mengi sana” alisema Dkt. Abbasi.
Dkt. Abbasi amesema kuwa
wameanzisha kituo ambacho kitatoa programu mbalimbali za michezo ili kuendana
na hali halisi ya sekta ya michezo na kuwafanya wataalamu wa michezo wakiwemo
wachambuzi, walimu wa michezo na waamuzi kuwa na mawanda mapana katika michezo
hatua inayosaidia kuendana na hali halisi ya michezo kwa mujibu wa Shirikisho
la Michezo Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la
duniani (FIFA).
Aidha, Wizara kupitia chuo cha
Maendeleo ya Michezo Malya imesaini Mkataba wa Ushirikiano (MOU) na Shirikisho
la Soka nchini (TFF) hatua itakayosaidia kuanzisha na kufundisha programu
mbalimbali za michezo zinazoenndeshwa na TFF ili kuleta uhalisia katika uendeshaji
wa shughuli za michezo nchini.
Dkt. Abbasi amewasisitiza
waajiri, watu binafsi, wachambuzi wa michezo mbalimbali na wadau wa soka na
michezo mingine kuwa Kituo cha Malya Dar es salaam katika jijini la kibiashara
na kukitumia ili kupata taaluma na ujuzi na kuwa na nchi ya watu wanaosema na
kutenda ili kuwa na maendeleo endelevu.
Zaidi ya hayo, Kituo cha Maendeleo ya Michezo Malya cha jijini Dar es salaam kitatoa pia fursa kwa wataalamu wa michezo waliopo jijini humo kushirikiana na chuo hicho ili kuleta tija katika sekta ya michezo.
0 comments:
Post a Comment