Muendelezo wa kampeni unaofanywa na mgombea wa ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia chama cha mapinduzi Dkt Angeline Mabula umewashawishi wapinzani kujiunga na chama hicho.
Akiwa kata ya Bugogwa viwanja vya Kilimantemi na Koroto Mhe Dkt Angeline Mabula akapata fursa ya kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo amesema kuwa sekta ya elimu imeboreshwa na shule mpya zimejengwa tatu za msingi ikiwemo Ihalalo, Bezi na Kayenze ndogo, Mbili za sekondari ikiwemo Kisundi na Kayenze na mbili za kidato cha tano na sita ikihusisha Buswelu na Sangabuye, Wakati shule kongwe za Bwiru wavulana na wasichana zikipokea fedha kutoka Serikali kuu kwaajili ya ukarabati.
Dkt Mabula akaongeza kuwa sekta ya ardhi jimbo lake limekuwa likifanya vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo likiongoza katika mpango wa urasimishaji wa makazi na umiliki wa ardhi sanjari na kutatua migogoro yote ya ardhi kwa zaidi ya asilimia tisini iliyokuwa ikisumbua jimboni humo
' Katika suala la umeme kama mnavyojua Ilemela ni manispaa hatukustahili kunufaika na mpango wa REA, Lakini Serikali sikivu ya Rais Dkt Magufuli ikaridhia katika mitaa 171tuliyonayo bado mitaa 56 tu ambayo haijapata umeme ba awamu hii inaenda kupata ' Alisem
Aidha mbali na kumshukuru Rais wa Serikali ya awamu ya tano Mhe Dkt John Magufuli kwa kutoa fedha za kuboresha sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya na vituo vya afya vya Karume na Buzuruga akapata wasaa wa kuwahimiza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kujiunga na huduma za bima ya afya ya gharama nafuu kama watashindwa bima ya NHIF.
Utekelezaji huo wa shughuli za maendeleo uliofanya na Serikali ya awamu tano chini ya Dkt John Magufuli, Mbunge Dkt Angeline Mabula na madiwani wa CCM ndio uliomshawishi Ndugu Mfungo Pamba aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wazee kata ya Bugogwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kuamua kurudi CCM na kupongeza uhodari wa viongozi hao katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo hivyo kujiunga na chama hicho papo hapo mara baada ya kuridhishwa na namna ya ujenzi wa nchi unavyokwenda.
0 comments:
Post a Comment