Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bwana Gerald Kusaya akihutubua Wakulima na Wageni walioshiriki kwenye hafla ya
uzinduzi wa kiwanda cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato (Chato Cooperative
Union – CCU Ltd) leo mchana, tarehe 9 Oktoba, 2020 wilayani Chato.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel akihutubia Wanaushirika na Wananchi wa wilaya ya Chato walioshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Chama Kikuu cha Ushirika Chato mchana leo mchana, tarehe 9 Oktoba, 2020.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bwana Justine Japhet akihutubia Wanaushirika na
Wananchi wa wilaya ya Chato walioshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Chama
Kikuu cha Ushirika Chato mchana leo mchana, tarehe 9 Oktoba, 2020.
Wanachama wa Chama Kikuu cha
Ushirika Chato wakicheza ngoma kusheherekea hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha
kuchakata pamba wilayani Chato, leo mchana, tarehe 9 0ktoba, 2020.
Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya awapongeza Wanachama wa Chama Kikuu cha
Ushirika wilaya ya Chato kwa kufufua kiwanda cha kuchakata pamba; Kiwanda
kilichosimama kwa zaidi ya miaka 20.
“Nawapongeza kwa
kuwa mmefufua kiwanda chenu na kwa kufanya hivyo, mmeunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dtk. John Joseph Pombe Magufuli
ambapo amedhamilia kuifanya Tanzania iwe nchi ya tofauti.”
Huu ni mwanzo
mzuri na Wanaushirika wa Chato hamjatuangusha, na hii ni ishara kuwa huko
tuendako ni kuzuri”. Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Aidha; Katibu
Mkuu Kusaya ametoa pongezi kwa uongozi wa wilaya ya Chato, uongozi wa mkoa wa
Geita kupitia Mkuu wa mkoa Mhandisi Robert Gabriel pamoja na uongozi wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bwana Justine Japhet
kwa kufanikisha mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 4 ambapo sehemu ya fedha
hizo, ilitumika kukarabati mashine za kiwanda hicho.
Katibu Mkuu
Kusaya ametoa wito kwa Wanachama wa Chama Kikuu cha Chato kuzalisha pamba zaidi
ili uwepo wa kiwanda uwe na faida zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.
“Ndugu zangu
Wakulima, tunawajibika kuongeza tija na uzalishaji wa pamba; Tumeambiwa uwezo
wa mashine za kiwanda hiki ni kuchakata pamba kiasi cha kilo milioni 30 wakati
ambapo uzalishaji wetu ni kilo milioni 8 hadi 12. Nataka niwahakikishie kuwa
uwezo huo tunao, ni suala la maamuzi tu”.
“Nimeelezwa pia
Wilaya ya Chato na Bihalamulo mnazalisha pamba safi na ya daraja la juu; Nitoe
wito muanze kuzalisha kwa tija na mara dufu, uzalishaji uwe juu na si kilo 200
kwa eka za sasa, bali mzalishe kuanzia kilo 1,200. Uzalishaji huu unawezekana
ikiwa mtatumia mbegu bora, mbolea, viuatilifu pamoja na Wataalam”.
“Jambo hili
limewezekana kwa Wakulima wengine kwa nini kwenu lishindikane? Kwa msaada wa
Wizara ya Kilimo, tutawasaidia kufika kwenye uzalishaji huo”. Amesisitiza
Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo ametumia nafasi hiyo kutoa agizo kwa Mkurugenzi wa Bodi ya
Pamba kuhakikisha inasaidia kwenye kuongeza tija na uzalishaji kwa Wakulima
wote nchini ili kutoa uzalishaji wa mwaka huu wa tani laki (120,000) ili
uzalishaji urudi kama mwaka juzi; Tani laki (300,000) na hadi mwaka 2025 ufike
tani laki (500,000).
Wakati huo huo
Katibu Mkuu Kusaya amewakumbusha Wanachama wa Vyama vya Ushirika kote nchini
kuendelea kutunza mali za Ushirika.
“Wanaushirika
hizini mali zetu; Mnapaswa kuzitunza, zilipatikana kwa jasho kupitia Wazazi
wenu na ninyi mnawajibika kuzitunza”. Amekaririwa Katibu mkuu.
Katibu Mkuu
Kusaya ameongeza kuwa kila mali ya ushirika iliyochukuliwa isivyo hali,
itarudishwa, zoezi la kurejesha mali za ushirika zilizoporwa lilianza mwaka
2016 kwa kusimamiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa Kassim Majali na kwa litaendelea kuwa endelevu.
0 comments:
Post a Comment