METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 23, 2020

DC BUKOBA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, AMALIZA MGOGORO ULIODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA 22

Mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiongea na wananchi wa kata Nshambya Manispaa ya Bukoba juu ya utatuzi wa mgogoro wa viwanja uiodumu kwa takribani miaka 22. Uliokuwa ukipelekea nyumba zaidi ya 374 kubomolewa na kuwaacha wenyenazo kukosa makazi.

Wananchi wa Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba wakimshangilia na kumpigia makofi mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro baada ya kutangaza uamui wa kufuta ramani ya zamani na kuzuia kubomolewa kwa nyumba za wananchi.

Mgogoro wa viwanja katika mtaa wa Kyebitembe Kata Nshambya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera uiodumu kwa miaka zaidi  ya miaka 22 na kusababisha kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani sasa umemalizika baada ya serikali kuingilia kati..

Akiongea katika  mkutano wa hadhara oktoba 21, Mwaka huu na wananchi wa kata hiyo, Mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amesema kuwa  halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kupitia kwa viongozi wake waliomaliza muda wao wakiongozwa na mstahiki Meya walipanga kubomoa nyumba za wananchi 374 pamoja na misingi kwa kosa walilolifanya wao awali.

Ameeleza kuwa serikaliya awamu ya tano ni serikali ya wanyonge hivyo haipo tayari kuona wananchi wake wakiteseka na kuhangaika kwa makosa ya wataalamu waliokuwa wanahusika na masuala ya ardhi ambao walikuwa wakiuza kiwanja kimoja kwa zaidi  ya watu wawili na kusababisha migogoro.

“Mimi nimeletwa Bukoba na Mhe. Rais kwaajili ya kuwahudumia wananchi na sio kuona wananchi wakiteseka, mgogoro huu umedumu kwa miaka 22 na kuna watu wamekuwa wakinufaika na mgogoro huu bila kujali wananchi wanaoumia, sasa kuanzia sasa nafuta ramani ya zamani ili ichorwe ramani mpya ambayo itaendana na halihalisi ilivyoya makazi ya sasa na kuanzi sasa pia hakuna kubomoa wala kugusa nyumba yoyote iliyojengwa hata msingi.” Ameeleza Kinawiro.

Ameongeza kuwa wale wote waliokuwa wakilalamikia viwanja ambavyo tayari viliuuzwa na waliouziwa wameshajenga halmashauri iwatafutie viwanja vingine ndani ya muda mfupi na wale waliokwisha jenga waachwe waendelee na maisha yao.

Aidha awetaka wananchi kwa kushirikiana na kamati ya urasimishaji walioichagua wenyewe wafanye mchakato wa haraka wa kuchanga pesa kwaajili ya kupimiwa viwanja vyao kwa wakati na kuwawezesha kupata  hati ili kila mmoja awe na umuliki unaotambuliwa kisheria.

Mara baada ya mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati   ya urasimishaji Ndg, Fakharudini Nuru  amemshukuru mkuu wa wilaya kwa maamuzi aliyoyafanya na kueleza kuwa migogoro hiyo imekuwa ikiathiri  shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kuwa wananchi walikuwa wakiishi kwa marumbano.

Fakharu ameongeza kuwa ataendelea kuwahamasisha wananchi wenzake ili waweze kuchanga fedha zitakazo wawezesha kupimiwa viwanja vyao na hatimaye kupata hati miliki na kuweza kuondokana na migogoro isiyo ya lazima.

Kwaupande wake Kaimu kamishina wa Ardhi mkoa wa Kagera Erick Makundi amesema kuwa baada ya serikali kufutilia mbali ramani ya zamani na hati zote zilizokuwepo amewataka wananchii hao kufata utaratibu kabla  hawajanunua viwanja wala kuanza ujenzi, na kuongeza kuwa endapowatawahi kuchanga pesa za ulasimishaji basi watapewa kipaumbele cha kupimiwa na suala la kupewa hati miliki halitazidi wiki mbili.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufui mnamo tarehe 16 mwezi septemba akiwa katika mkutano wa kampeini mjini Bukoba aliagiza serikali ya wilaya Bukoba kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa viwanja Kyebitembe mapema mwaka huu ili kuwawzesha wananchi kuishi kwa uhuru na usalama.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com