METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 13, 2020

Wadau wa Kilimo cha Mboga mboga na Matunda waitaka serikali kuwekea mkazo kilimo hicho


Pichani:Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha wakipatiwa mafunzo na Mtaalam wa masuala ya Kilimo cha Mboga Mboga na Matunda Mkoani Hapo (Picha na Agnes Geofrey)

Na Agness Nyamaru.

Serikali imetakiwa kuweka mkazo katika Kilimo Cha mbogamboga na matunda ili kuongeza ajira kwa watanzania waweze kutumia fursa ya kujipatia kipato na kuondokana na umaskini kwani kilimo hicho kimeonekana kuwa chini katika nchi ya Tanzania.

Akizungumza Wilayani Arumeru mkoani Arusha katika mafunzo yaliyofanyika kwenye taasisi ya kimataifa ya utafiti na uendelezaji wa mboga za majani kurugenzi ya mashariki na kusini mwa Afrika kwa waandishi wa habari kutoka mkoa wa Dodoma na Arusha Dkt Gabriel Rugamela alisema mafunzo hayo yamelenga kuelimisha jamii na kuleta tija katika sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda na kujua umuhimu wa kilimo na kutumia mbogamboga Kama sehemu ya lishe katika jamii.

Aidha alisema watu wengi hawatumii mboga Kama sehemu ya lishe badala yake hutumia kwa kukosa kipato kwani zipo changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ikiwemo elimu,ukosefu wa miundo mbinu ya kilimo ,kanuni na taratibu za tozo na uhaba wa wataalam.

Kilimo cha mbogamboga ikiwemo upatikanaji wa masoko na miundombinu kwa wakulima vinayokwamisha uendelevu wa kilimo hicho, uwepo wa wataalamu wachache hali inayosababisha uzalishaji mdogo wa mbogamboga hizo pamoja na elimu ndogo kwa wakulima juu ya kutumia fursa itokanayo na kilimo hicho.

"Pamoja na changamoto hizi tunaiomba serikali kutanua sekta ya kilimo cha mbogamboga kwa kuweka mikakati itakayoendeleza kilimo hichi kwa kuweka mkazo na kutambua thamani yake"alisema Rugamela.

Mkurugenzi mtendaji wa Taha Dkt Jacqueline Mkindi alisema sekta ya hortculture imeendelea kukua kwa kasi kwani wanawajengea wakulima uwezo wa kushiriki katika hatua za kuchagua mbegu bora,huku wakijiunga pamoja na world Vegetables ili kuendelea kutunza sekta ya kilimo na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.

"Tunatengeneza ratiba ambayo inatoa mafunzo ya muda mfupi  kwa wale wanaomaliza vyuo vikuu na kwa wafanyabiashara wambogamboga Ili kupata wawekezaji katika kutoa huduma mbalimbali kwenye sekta hiyo alisema Mkindi" 

Aidha Mkindi alisema jukumu kubwa ni kuhakisha mazao yanafika Tanzania na kwenye masoko yakimataifa ya ndani na nje  kwa kuwajengea wazalishaji Uwezo kulingana na mahitaji ya masoko.

"Sisi tumejikita sana kwaajili ya kufungua masoko ya ndani na kimataifa na katika kuzungumza  na wadau mbalimbali kwa kujaribu kuuza bidhaa za kitanzania ili kuweza kupata tenda ya Usambazaji katika masoko hayo alisema Mkindi"

Kwa upande wake Meneja mauzo na masoko kutoka katika Kampuni ya uzalishaji mbegu ya East West Bi.Edilitruda Temba alisema kuwa kupitia kampuni yao waliweza kuwafikia asilimia 85 ya wakulima kwa kuwapatia elimu ya kilimo itakayo wasaidia kulima kilimo chenye tija kitakacho kubalika sokoni na kumuingizia kipato.

"kutokana na changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wakulima wa kilimo cha mbogamboga na matunda,kampuni yetu imejikita kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa mbogamboga katika jamii kwa kuzingatia ubora wa mbegu."alisema temba.

Nae mmoja wa watafiti kutoka kitengo Cha benki ya mbegu Jeremiah Sigilla alisema tangu 1992 kuanzishwa kwa kituo hicho ,benki hiyo ilianza kukusanya mbegu za mbogamboga ili kuzitunza na kusaidia katika uchakataji wa mbegu bora kwani ni benki iliyobeba vinasaba ikiwa na lengo la kutunza utofauti wa rangi,radha,uwezo wa kuhimiri ukame na magonjwa.

Mbegu Bora lazima iwe ina uwezo wa kuzaa na kuwa na ukinzani wa kuhimili magonjwa ,wadudu,Hali ya hewa ili mmea usiweze kukauka,kwani wanachukua  viambata na kupelekea kwenye mbegu nyingine ili kupata mbegu bora zaidi ambayo ina manufaa na wakulima wanaipenda kutokana na kuhimili mazingira yote.

Sigilla aliongeza kuwa changamoto wanazozipata ni ushirikiano kwa baadhi ya wataalam na almashauri katika kuwafikia wakulima ili kutoa elimu,hivyo wakulima wengi wanapata hasara kutokana na kushindwa kutambua nyakati za masoko ya mbogamboga wanazozilima.

"Ili tuwe na usalama wa chakula katika nchi lazima tuwe na utofauti wa chakula,kwani utofauti huo husaidia katika majanga pindi yatakapo tokea Kama ukame ,mafuriko ili kuweza kusaidia wakulima na kukusanya mbegu"alisema Jeremiah Sigilla

Sambamba na hayo mmoja wa wanufaika wa mradi wa kilimo biashara Agness Ndosi alisema hapo mwanzo walikuwa wanapata changamoto nyingi  ya masoko Hali iliyopelekea  kupata kipato kidogo lakini walipopata  elimu kutoka shirika la world vegetables kipato kikaongezeka.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com