Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika Kijiji cha Mlamleni wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwasili katika Kijiji cha Mlamleni ili kuwasha umeme. Wa Pili kulia ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa vitongoji vya Kisasa na Churwi mara baada ya kufika katika Vitongoji hivyo kukagua kazi ya usambazaji umeme.
Na Hafsa Omar, Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu, ameendelea kukagua utekelezaji wa kazi ya kusambaza umeme vijijini
pamoja na kuwasha umeme katika vijiji mbalimbali nchini ili
kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo mwaka
2021.
Tarehe 16 Septemba, 2019, alikagua
kazi ya usambazaji umeme katika vitongoji vya Kisasa na Churwi pamoja na
kuwasha umeme katika kijiji cha Mlamleni Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa
Pwani.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Mlamleni, Naibu Waziri alieleza kuwa wakandarasi wakikamilisha
miradi ya umeme na kukabidhi kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),
wananchi wataunganishiwa kwa bei ile ile ya shilingi 27,000.
Aliwaahidi wananchi wa kijiji hicho
kuwa, umeme utasambazwa kwa wananchi wote kwani Tanesco inahitaji wateja ili
Shirika hilo liweze kujiendesha lenyewe, hivyo ni lazima wateja wengi
wapatikane.
Naibu waziri alisema kuwa, Wilaya ya
Mkuranga ni moja ya wilaya ambazo zipo kwenye mradi wa umeme wa ujazilizi awamu
ya pili (A) utakaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo maeneo
mengi zaidi yataunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000.
Vilevile, alisema kuwa, wilaya hiyo
itasambaziwa umeme kupitia mradi wa Peri-Urban ambapo wananchi 4293 ambao ni
wateja wa awali wataunganishwa.
0 comments:
Post a Comment