Katika hafla ya kukabidhi matundu manane ya vyoo kwa kila shule yaliyojengwa na shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania Mradi wa Bushangaro AP kwa serikali ya mkoa,meneja wa shirika hilo kanda ya Kagera Juliana Charles amesema kuwa walifika katika shule hizo na kusikitishwa na hali waliyoikuta na kuwiwa kuanzisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Juliana amesema kuwa shirika hilo linajihusisha Zaidi na makuzi ya mtoto hivyo kujenga miundombinu ya vyoo mashuleni ni moja ya huduma muhimu kwa mtoto ambayo itampelekea kusoma kwa raha lakini pia kuweza kumuepusha na magonjwa mbali mbali ya mlipuko yanayoweza kumtokea.
Sambamba na ujenzi wa vyoo hivyo shirika hilo pia limekabidhi mradi wa maji ambayo mtandao wake umesambazwa kwenye vijiji viwili ambavyo vipo kata ya Bushangaro na kuweza kusambazwa katika zahanati ya Nyakagoyagoye ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kwa jamii ya wanakaragwe.
Katibu Tawala wa mkoa Kagera Profesa Faustine Kamzora baada ya kukabidhiwa miradi hiyo ameitaka jamii kuitunza miradi na kutunza mazingira ili kuhakikisha ubora wa miradi unabaki ulele ule ambapo pia ameutaka uongozi utakaosiamamia mradi wa maji kuhakikisha maji hayo wanayatibu kabla ya kumfikia mwananchi ili kumuepusha na magonjwa.
Kamzora amesema mradi umejingwa kwa ufadhili wa nchi ya Ujerumani kwa garama ya zaidi ya shilingi milioni 400 na endapo Mazingira ya miundomibun ya maji yakiwekwa kwenye hali ya usafi unao zingatia matunzo bora unaweza kuondoa magonjwa yanatokana na matumbo hasa kwa watoto wadogo.
Aidha Kamzora almesema,vituo vya afya na Hospitali na zahanati kwa asilimia kubwa zinapokea matatizo ya magonjwa ya upungufu wa maji kwa asilimia 70 pamoja nna magonjwa ya tumbo kutokana na watu kutumia maji ambayo sio salama ambayo yote hayo ni ukosefu na uhaba wa maji yenye uhakika .
“ pia maji yanafaida nyingi na sio kuondoa magonjwa ya tumbo na upungufu wa maji mwili pekee bali na kuanzisha bustani majumbani na kujipatia lishe bora ya watoto lakini pia matumizi mengine ya nyumbani ikiwemo kufua na kufanyia usafi mwingine”amesema Kamzora.
Meneja wa shirika la Worldvision kanda ya Kagera Juliana Charles amesema mradi huo utahudumia wananchi ambao awali walikuwa wakitumia muda mrefu kufuata maji vijiji jirani ambayo bado yalikuwa hayapo katika usalama.
Charles amesema kuwa,”baada ya kupatiwa taarifa na kamati ya maji kijijini hapo, shirika liliweza kufika eneo la chanzo na kufanya tathimini ya shughuli ya ujenzi utakaoweza kuzua mifugo isiweze kuingia ndani ya maji hayo kwa kuyazumguzisha, .
Shirika limefanya ujenzi wa chanzo kwa kujengea maji ikiwa ni kuzuia mifugo,na kutunza chanzo kisiweze kuharibiwa na jamii ambayo inatakiwa yenywe itunze chazo hiki”.
Mwenyekiti wa kjiji cha Nyakagoyagoye Salmoni Mtilani alisema, kukamilika kwa ujenzi huo utaondoa watoto kutumia muda mwingi kutafuta maji na wakati mwingine kutokuhudhulia shuleni kwa ajiri wazazi wao kuwatuma maji umbari mrefu
“ Sio watoto sio wazazi wao wanatembea umbari mrefu wa kilomita18 kwenda kijiji jirani kufuata maji ambayo hayachangamani na mifugo kijingine watoto kutohudhulia shuleni kabisa na kuwafanya kukosa masomo na hatimaye kushuka kitaaluma” Amesisitiza Mtilani
Mtilani alisema, kuwa kijiji cha Nyakagoyagoye kilikuwa kinafuata maji kijiji jirani kwa sababu chanzo ambacho kimefanyiwa ujenzi wanajamii walikuwa wanayatumia kama maji ya mifugo kwa mazinmgira yalikuwa hayalidhishi kwa wanajamii kwenda kuchota maji hayo.
0 comments:
Post a Comment