METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 2, 2020

WANAMONDULI HAKIKISHENI CCM INASHINDA-MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja Barafu uliopo Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo, Septemba 2, 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Zelote Stephene . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua kampeni za CCM wilayani Monduli kwenye uwanja wa Barafu Mto wa Mbu , Septemba 2, 2020. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa vazi la CCM na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa wakati alipozindua kampeni za CCM wilayani Monduli katika uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, Septemba 2, 2020. Kulia ni Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Monduli Fred Lowassa, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM wilayani Monduli kwenye uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, Septemba 2, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa  na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimnadi Mgombea UbungeJimbo la Monduli, Fred Lowassa wakati alipozindua Kampeni za CCM wilayani Monduli, Septemba 2, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amevunja makundi ya wanachama wa CCM walioomba uteuzi wa kuwania ubunge katika jimbo Monduli mkoani Arusha na kuwataka washirikiane katika kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.

 

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo amewaomba wakazi wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha na Watanzania wote bila kijali itikadi zao wamchague Rais Dkt John Pombe Magufuli ili aendeleze kazi ya kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.

 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 2, 2020) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Monduli, Arusha kwenye mkutano wa kampeni za CCM kumuombea kura Rais Dkt. Magufuli pamoja na wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa CCM.

 

“Kazi iliyonileta hapa ni kuwaomba kura wana Arusha na wanaMonduli naomba kura zenu zote bila ya kujali itikazi za vyama vyenu tumpigie kura Mheshimiwa Rais Magufuli na mgombea ubunge Fredrick Lowassa na wagombea wote wa udiwani kupitia CCM.”`

 

Amesema wananchi wanajua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli, hivyo amewaomba wamchague tena kwa kuwa miradi mikubwa ya kimkakati aliyoitekeleza kwenye maeneo mbalimbali nchini imegusa wananchi wengi.

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 imeweka msisitizo kwa Serikali kuleta mageuzi ya utalii, kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.

 

“Tutahakikisha uzalishaji unaongezeka katika sekta ya mifugo, utalii na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuchochea maendeleo ya uchumi, hasa katika sekta za viwanda na huduma za jamii. Fugeni kisasa mpate faida na Serikali ya CCM itaendelea kuwaunga mkono.”

 

Amesema tayari vijana wengi wamenufaika kupitia sekta hizo, hivyo ni lazima Serikali iendelee kuziboresha zaidi. Pia Serikali imepanga kuongeza idadi ya watalii wanaoingia pamoja na kuongeza pato litokanalo na sekta hiyo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com