Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Chizumbi Kata ya Ukwile Leo Tarehe 13 Septemba 2020.
Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga akicheza wimbo maalumu wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura wakati alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Chizumbi Kata ya Ukwile Leo Tarehe 13 Septemba 2020.
Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji na Kata ya Ukwile Leo Tarehe 13 Septemba 2020.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Fatuma Mnahwate akimnadi Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji na Kata ya Ukwile Leo Tarehe 13 Septemba 2020.
Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Chimbuya Kata ya Ukwile Leo Tarehe 13 Septemba 2020.
Na Mwandishi Wetu-Songwe
Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa mkoani Songwe Japhet Hasunga amesema kuwa ndege zilizonunuliwa na serikali ni kwa ajili ya kufanya biashara na kuingiza Pato la nchi.
Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 13 Septemba 2020 wakati wa mikutano ya kampeni katika kijiji cha Chizumbi, Ukwile na Chimbuya ya Kwanza Kata ya Ukwile ambapo amewapongeza wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Amesema kuwa wapo wanasiasa wasiokuwa na mapenzi mema na nchi yao wamekuwa wakiyatangaza vibaya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege kwa madai kuwa ndege hizo hawawezi kupanda masikini.
"Ni kweli kabisa masikini hawezi kupanda ndege na dhamira ya serikali kununua ndege tulitaka zifanye biashara ili kipato kinachopatikana kiweze kuwahudumia wananchi kwa kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu na michezo" Alisisitiza Hasunga
Hasunga amewataka watanzania kumuunga mkono mgombea urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli, Wabunge na madiwani wa CCM nchi nzima.
Amesema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Magufuli mwaka 2015 zimetekelezwa kwa kiasi kikubwa hivyo wajibu wa wananchi ni kuendeleza heshima ya CCM kwa kuwachagua wagombea wote wanaotokana na chama hicho.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment