METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 12, 2020

Chagueni Mafiga matatu kwa CCM Kwa ajili ya maendeleo-Hasunga

Mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kampeni katika kijiji cha Manyara kilichopo Kata ya Hasamba Mkoani Songwe, leo Tarehe 12 Septemba 2020.

Sehemu ya wakazi wa Kijiji cha Migombani Kata ya Hasamba Mkoani Songwe wakimlaki Mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kampeni, leo Tarehe 12 Septemba 2020.

Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Japhet Hasunga wakati wa kampeni katika kijiji cha Iyika kilichopo Kata ya Hasamba Mkoani Songwe, leo Tarehe 12 Septemba 2020.

Mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kampeni katika kijiji Itika kilichopo Kata ya Hasamba Mkoani Songwe, leo Tarehe 12 Septemba 2020.

Mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndg Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Mbozi mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, leo Tarehe 12 Septemba 2020.

Na Mwandishi Wetu, Songwe

Chama cha Mapinduzi Mkoani Songwe kimewataka wananchi kumchagua Mgombea Urais wa CCM Ndg John Pombe Magufuli, Wabunge pamoja na madiwani wote wa CCM.

Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni katika kijiji cha Migombani, Iyika, Manyara Kata ya Hasamba mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa kupitia tiketi ya CCM Ndg Japhet Hasunga amesema kuwa ili kuongeza chachu ya maendeleo nchini watanzania wanapaswa kuichagua CCM kwani imebeba ajenda ya maendeleo kwa watanzania.

Amesema kuwa kutokana na kazi kubwa alizozifanya Rais Magufuli anahitaji kulipwa na watanzania kwa zawadi ya kura nyingi kwani kufanya hivyo kutaongeza imani kwake kwa wananchi anaowaongoza.

Hasunga amesema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Magufuli zimetekelezwa kwa kiasi kikubwa ambapo amejitahidi kufanya kazi nzuri zaidi ya ahadi alizotoa hivyo kufanya kazi kubwa zaidi ya zile zilizoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Kuhusu sekta ya Kilimo Hasunga amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli imehakikisha masoko ya kahawa yanahamia kwenye kanda zinazoongoza kwa uzalishaji badala ya kuwa na soko moja lililokuwa likifanyika Mjini Moshi pekee badala yake kwa sasa inafanyika kwenye kanda mbalimbali na Songwe ikiwemo.

Ameongeza kuwa wakulima kote nchini wameendelea kuneemeka na punguzo la bei za mbolea ya kupandia na kukuzia kwani serikali imeendelea kusimamia kwa weledi mkubwa upangaji bei za mbolea ili kuwarahisishia wakulima.

Kadhalika amesema kuwa serikali ya Rais Magufuli imesimamia kwa weledi mkubwa upatikanaji wa Pemebejeo za kilimo kwani zamani pembejeo  zilikuwa zinachelewa kuwafikia wakulima lakini kwa sasa Pembejeo zinafika kwa wakati.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com