Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akiangalia na kupata ufafanuzi kutoka kwa Meneja Mwajiri wa kiwanda cha Good Will Bw.
Figa Msaphiry juu ya marumaru zinazotengenezwa kiwandani hapo
alipotembelea kukagua na kuzungumza na wawekezaji hao Juni 29, 2019
Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akiangalia namna vifungashio vya marumaru vinavyotengenezwa katika
kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
pamoja na viongozi wa Halmashauri alioongozana nao katika ziara yake
kujionea namna marumaru zinavyotengenezwa katika kiwanda cha Good Will Limited kilichopo Mkuranga Pwani.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya ziara yake
kiwandani hapo.Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will
akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
alipotembelea kiwanda hicho Mkoani Pwani.Afisa Ufuatiliaji Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Moureen Guveti akichangia chambo wakati wa kikao hicho.Baadhi
ya wajumbe wa kikao walioshiriki ziara hiyo wakimsikiliza Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo
pichani) wakati wa kikao cha pamoja cha majumuisho mara baada ya
kumaliza ziara yake kiwandani hapo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………..
NA.MWANDISHI WETU – OWM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchi Mhe. Angellah Kairuki
ameutaka uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha GoodWillTanzania ceramic ltd kuzingatia
ustawi wa wafanyakazi wake kwa kuzingatia kanuni na sheria mbalimbali
za ajira nchini ili kuendelea kuwa mazingira mazuri ya wafanyakazi wake.
Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake
mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo katika Kijiji cha Mkiu
kata ya Nyamato Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Waziri Kairuki alieleza kuwa, upo umuhimu
wa kujali wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi kwa kuzingatia usalama
na afya mahala pa kazi ili kuondokana na mazingira mabaya yanayoweza
kukwamisha uzalishaji unaotarajiwa.
“Ikiwa kiwanda kimeweza kutoa ajira
zipatazo 3000 ni idadi kubwa hivyo lazima myatazame mahitaji yao na
kuendelea kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi wawapo
kazini,”Alisema Waziri Kairuki.
Aliongeze kuwa miongoni mwa maeneo muhimu
kwa wafanyakazi wenu ni kuhakikisha mnawapa mafunzo kazini ili kuongeza
ujuzi katika fani mbalimbali zinazoendana na uzalishaji kiwandani hapo.
Aidha aliwataka kuendelea kuwapa motisha
na kuwa na njia za ubunifu katika kuhakikisha kila mfanyakazi anakuwa
mwenye ustawi na kufurahia mafanikio ya uwepo wa kiwanda hicho.
“Ni lazima kujali masuala ya usalama wa
afya zao wawapo kazini, kujali stahiki zao, kuwapa kazi zenye staha kwa
kulingana na kanuni na sheria za kazi zilizopo,”alisisitiza Waziri
Kairuki
Naye Meneja Mwajiri wa kiwanda hicho Bw.
Figa Msaphiry alimpongeza Waziri kwa Ziara yake kiwandani hapo na
kuahidi kuendelea kuyatekeleza maagizo hayo ikiwemo la kuhakikisha
wanaendelea kujali masuala ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi kwa
kuzingatia mchango unaotolewa na wafanyakazi hao katika kiwanda hapo.
Alifafanua kuwa, kiwanda kimefanikiwa
kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania 936 kati ya hao
wanaume 887 na wanawake 49, lakini pia kiwanda kimetengeneza ajira
zisizo rasmi Zaidi ya 1,500 na kwa siku wanapokea vibarua ambao wapatao
40 hadi 50 na hii kupeleekea kuongeza fursa za ajira nchini.
Aliongeze kuwa wafanyakazi wamechangia
matokeo chanya katika uzalishaji ambapo kiwanda kinazalisha marumaru
mita za eneo 40,000 mpaka 50,000 kwa siku kuwa ambapo soko la ndani ni
kwa asilimia 30 hadi 40 na soko la nje ni kwa asilimia 60 hadi 70.
“Kiwanda chetu kimeweza kupanua soko la
marumaru kwa kuuza katika nchi za nje, kwani kwasasa kiwanda kinauza
marumaru katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Congo kwa
kuzingatia ubora wa bidhaa zetu,”alieleza Figa .
kiwanda cha Good Will Company Limited
kilijengwa mwezi Machi, 2016 na kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa
kiwanda hiki na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa Kasimu Majaliwa, na kuanza uzalishaji wake mnamo Mwezi Aprili
Mwaka 2017.Kiwanda kinazalisha marumaru za sakafuni (floor tiles) na
marumaru za ukutani (wall tiles) kwa saizi zote na “scating”, Katika
uzalishaji wa marumaru kiwanda kinatumia malighafi tofauti tofauti
ambapo 95% ni malighafi toka hapahapa Tanzania na 5% kutoka China ambazo
ni kemikali.Malighafi zinazotoka Tanzania ni felidisper ambayo inatoka Tanga – Handeni, Morogoro na Dodoma, nyingine ni Soap stone kutoka Dodoma na Morogoro, Magnesite kutoka Same Moshi, Udongo wa mfinyanzi (clay soil) na udongo mwekundu (red soil) kutoka Mkuranga – Pwani, Limestone kutoka Mavuji – Kilwa na Kaolin kutoka Kisarawe Pwani. Mradi huu wa ujenzi wa kiwanda umegharimu jumla ya fedha za kigeni dola milioni 50.
0 comments:
Post a Comment