METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 8, 2020

WAZIRI MKUU APONGEZA UJENZI WA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA UNAOTEKELEZWA NA NFRA

Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa akitoa maelezo ya kuhusu uhifadhi wa nafaka mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.  (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa akitoa maelezo ya kuhusu uhifadhi wa nafaka mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mfano wa gunia la mahindi wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amepongeza ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mradi unaotekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo tarehe 8 Agosti 2020 wakati alipotembelea Banda la NFRA kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi huo ni mahususi kwa ajili ya Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000. 

Akitoa taarifa ya Mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa amesema Mradi huo unajumuisha ujenzi wa vihenge 56 na maghala ya kisasa 9 ambavyo kwa pamoja vinaongeza uwezo wa kuhifadhi kwa tani 250,000. Kwa sasa Mradi huu umefikia umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Amesema Uhifadhi wa nafaka kwa kutumia maghala ya kawaida, akiba inaweza kuhifadhiwa kwa takriban miaka mitatu tu kabla ya kuanza kupoteza ubora. Kwa kutumia vihenge vya kisasa, akiba inaweza kuhifadhiwa hata kwa zaidi ya miaka mitano bila kupoteza kiwango cha ubora

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni Taasisi ya Umma chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa chini ya Sheria za Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2008.

NFRA ina jukumu kuu la kuhakikisha usalama wa chakula ndani ya nchi kwa kununua, kuhifadhi na kutoa chakula katika maeneo yenye upungufu na kwa waathirika wa majanga mbalimbali. 

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com