Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Grace Mwangwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga alipotembelea banda la Wizara na Taasisi zake katika Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kipindi cha kati ya mwaka 2015 mpaka 2020 imetoa mikopo yanye thamani ya shilingi Bilioni 63.5 ikiwa ni sehemu ya huduma za Wizara kwa jamii.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga katika Banda la Maonesho ya Wizara hiyo katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Waziri Hasunga ameeleza kufurahishwa kwake na huduma za Wizara na kuongeza kwa huduma hizo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwani ni Wizara muhimu katika kuhamasisha jamii kufanya kazi na kujiletea maendeleo yao wenyewe.
“Nyinyi Wizara na Taasisi zilizo chini yenu mnafanya kazi nzuri sana ya kuwaletea wananchi maendeleo mfano mikopo mnayoitoa, huduma za kisheria, usuluhishi wa migogoro ya ndoa na mambo mengine mengi” alisema
Waziri Hasunga ameongeza kuwa huduma za ushauri zinaisaidia jamii hasa masuala ya lishe kwa jamii kwa kuwa pamoja na kilimo, uvuvi lakini bado kuna tatizo la udumavu katika jamii zetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Grace Mwangwa amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Wizara imetoa mikopo inayofikia kiasi cha shilingi Bilioni 63.5 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali.
Adha amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, imeanzisha kamati zipatazo 16,343 kwa ajili ya kupambana na kutokomeza vitendo mbalimbali vya ukatili nchini.
Katika Maonesho hayo ya 27 ya Nanenane, Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imeshirikisha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Tasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Chuo cha Ufundi Misungwi pamoja na Wajasiriamali mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment