METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 25, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO KWA KULIPA KODI ZA SERIKALI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Jimbo lake kuwa waadilifu na wazalendo kwa kulipa kodi mbalimbali za Serikali

Mhe Dkt Angeline Mabula ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha Ziara yake kwa Kata zote za  Jimbo lake aliyoihitimishia katika Kata ya Nyamanoro kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara vwanja vya Mashishanga kwa kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa hapo kero mbalimbali za wananchi zikiwemo za Ardhi na Uhamasishaji wa Shughuli za Maendeleo ambapo pia amesisitiza juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa Serikali ili iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

‘… Hizi kodi tunazolipa ndizo zinazokwenda kufanya masuala ya maendeleo, Miundo mbinu tunayosema kwenda kujengwa haiwezi  kukamilika,Lakini tunawajibu sisi wenyewe niwaombe na hili tumekuwa tukilisema kuna zile kamati zetu kwenye halmashauri ikiwemo ile ya mipango miji ni lazima kuangalia wangapi wamelipa kodi na wangapi bado lifanyike mara kwa mara ili watu hawa wawe wamekumbushwa na hili liende sambamba na kodi zingine ndugu zangu …’ Alisisitiza

Aidha Mbunge huyo mbali nakutoa tofali kwaajili ya ujenzi wa shule ya watoto wa eneo hilo,kukemea matendo ya kinyama yanayofanywa matajiri kwa kuwanyang’anya ardhi na kuwanyanyasa watu masikini , kuelimisha wananchi wake juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji na kumiliki ardhi amezungumzia juu ya mradi mkubwa wa maji unaoenda kutekelezwa ndani ya Jimbo lake ukihusisha ujenzi wa matanki ya maji kwa maeneo ya Kitangiri, Nyasaka, Mjimwema na Kirumba huku akiwataka kuwa wavumilivu na wenye subira na ushirikiano katika kuhakikisha miradi hii inafanikiwa

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela akiwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Ndugu John Wanga mbali kutolea ufafanuzi wa maswali ya wananchi na kujibu baadhi ya kero wamemuhakikishia mbunge Dkt Angeline Mabula ushirikiano kuhakikisha wanamaliza changamoto za Ilemela

Nae Mwenyekiti mwenyeji palipofanyikia mkutano huo wa hadhara mtaa wa Nenetwa amemshukuru Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa kuamua kuitembelea kata ya Nyamanoro hasa kwenye mtaa anaouongoza na kuomba kufika tena kwa awamu nyengine kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wake zilizodumu kwa muda mrefu

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
26.08.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com